Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Afungua Kongamano la Afya na Maisha Bora Katika Viwanja vya Maisara Zanzibar

Mama Asha Suleiman,Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Mgeni Hassan Juma, Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali na Viongozi Serikali wakisubiri kumpokea Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuhudhuria Tamasha la Biashara la Nne linalofanyika katika viwanja vya Maisara na kufungua Kongamano la Afya na Maisha Bora. lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipowasili katika viwanja vya Tamasha la Maonesho linalofanyika katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwenamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Waziri wa Biashara Viwanda na Msoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Inaya Zanzibar Limited Cheherazade Cheikh akitowa maelezo ya bidhaa za manukato na sabuni zinazotengenezwa na kampuni hiyo ikitumia malihafi za Zanzibar. wakati wa maonesho ya Tamasha la Nne la Biashara katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwenamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Inaya Zanzibar Limited Cheherazade Cheikh akitowa maelezo ya bidhaa za manukato na sabuni zinazotengenezwa na kampuni hiyo ikitumia malihafi za Zanzibar. wakati wa maonesho ya Tamasha la Nne la Biashara katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZAIDAT cha Chukwani Zanzibar Tatu Suleiman, kinachijishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za vipodozi na sabuni.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZANAP Nassor Hamad Omar kinachojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za Majani ya Chai, wakati wa Tamasha la Moenesho ya Biashara Zanzibar linalofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.


Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Juma Ali Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Afya na Maisha Bora lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko lililofanyika katika viwanja vya Maoenesho ya Tamasha la Nne la Maonesho Zanzibar linalofanyika katika Viwanja vya Mpira Maisara.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akihutubia wakati wa Kongamano la Afya na Maisha Bora lililofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Tamasha la Nne la Biashara katika viwanja vya Maisara Zanzibar kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kulifungua Kongamano hilo.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.