Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa VIP katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kabla ya kuaza ziara yake ya Wiki Moja katika Nchi za Falme za Kiarabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo 21-1-2018, akielekea katika Nchi za Falme za Kiarabu kuaza ziara yake ya Kiserikali ya Wiki Moja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiongozana na Mumewe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kushoto Makamu wa Rais wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee wa CCM Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akiondoka Zanzibar kuelekea katika ziara yake ya Wiki Moja katika Nchi za Falme za Kiarabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuaza ziara yake ya Wiki Moja katika Nchi za Falme za Kiarabu.
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 20.01.2018
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameondoka nchini leo kwenda
nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ziara ya wiki moja kufuatia
muwaliko wa viongozi wa nchi za Umoja huo.
Ziara hiyo ya Dk. Shein inatarajiwa
kuanza kesho tarehe 21 na kumaliza tarehe 27 Januari mwaka huu katika nchi hizo
za (UAE), ambapo ataanza ziara yake kwa kufanya mazungumzo na Mtukufu Sheikh
Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri
Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) nchini Abu Dhabi.
Akiwa mjini Abu Dhabi
Dk. Shein atakutana na Mhe. Mohamed Saif Suwaid, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Maendeleo ya Abudhabi “Abudhabi Fund for Development”, atatembelea mji wa
Nishati, Masdar, atatembelea jumba la kumbukumbula Louvre, msikiti wa Shaikh
Zayed pamoja na sehemu ya kihistoria ya Wahat Al Karama.
Aidha,Dk. Shein afanya
ziara Dubai na kukutana na kufanya mazungumzo na Mtukufu Shaikh Mohammed bin
Rashid Al Makhtoum, Makamo wa Rais na Waziri Mkuu wa (UAE) na Mtawala wa Dubai.
Rais Dk. Shein akiwa
Dubai atatembelea Maeneo Huru na Bandari ya Jebel Ali, atakutana na Jumuiya ya
Wafanyabiashara, wawekezaji na wenyeviwanda wa Dubai na kutembelea Mji mpya wa
kisasa wa Nakheel pamoja na Mradi wa Palm Jumeirah.
Katika nchi hizo za
Umoja wa Falme za Kiarabu, Pia, Dk. Shein atafanya ziara mjini Sharjah na
kukutana pamoja na kufanya mazungumzo na Mtukufu Dk. Shaikh Sultan Mohammed Al
Qasimi, Mtawala wa Sharjah
Akiwa Sharjah, Dk. Shein
atatembelea katika eneo la shughuli za uvuvi la ‘East Fishing Processing LLC”,
atatembelea shamba la ngombe wa maziwa la Al Rawabi, pamoja na kutembelea mji
wa michezo wa Dubai.
Sambamba na hayo, Dk.
Shein pia, atafanya ziara Ras Al Khaimah na kukutana pamoja na kufanya
mazungumzo na Mtukufu Shaikh Saud Saqr Al Qasimi, Mtawala wa Ras Al Khaimah
pamoja na kutembelea eneo la Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa
Mafuta na gesi asilia ya Ras Al Khaimah
“Rak Gas”.
Katika
ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa
Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
Salama Aboud Talib, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Salum Mohamed,
Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Juma Ali Khatib, pamoja na Mshauri
wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed
Ramia Abdiwawa.
Wengine
ni Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Juma Ali Juma, Balozi
Mohamed Haji Hamza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Khamis
Nassor
na watendaji wengine wa Serikali.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa
kurejea nchini Jumamosi, tarehe 27 Januari, 2018.
Katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Dk. Shein aliagwa na viongozi
mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali, viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na
Usalama pamoja na wananchi ambao
waliongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment