Habari za Punde

Waziri Mkuu awasili nchini Ethiopia kushiriki Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Addis Ababa, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu cha kumbukumbu, cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi huyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.