Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Sheria Mawakili Watoe Elimu ya Sheria Kwa Wananchi wa Kijiji cha Donge Unguja.

Mmoja ya Mawakili akitoa ufafanuzi kuhusu Sheria ya ardhi kwa Wananchi wa Donge vijibweni  ambao wanamskiliza.
Wakili wa Serikali Hamisa Mmanga Makame akitoa elimu kwa Wananchi wa Donge vijibweni juu ya kupiga Vita udhalilishaji na Migogoro ya Ardhi

Wananchi wa Donge vijibweni wkilisiliza kwa makini wakati wakipatiwa Elimu  ya  udhalilishaji na Migogoro ya Ardhi ikiwa ni shamra shamra za maazimisho ya wiki ya sheria Zanzibar ambayo kilele chake ni Februari 12.Picha na Miza Othman – Habari Maelezo- Zanzibar.

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.       07/02/2018.
Katika kuadhimisha wiki ya Sheria Zanzibar, Mawakili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wameendelea kutoa elimu kwa Wananchi mbali mbali wa Vijijini ili kuzifahamu na kuzitekeleza vyema Sheria.
Mawakili hao wamewataka Wananchi kuifahamu vyema Sheria ya Ardhi na Sheria ya Mahakama ya Kadhi ili waweze kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo waliyasema jana walipokuwa wakitoa Elimu kwa Wananchi wa Donge vijibweni Wilaya ya kaskazini “B” Unguja  juu ya umuhimu wa kazi na majukumu yanayofanywa na Mawakili hao.
Wamesema  wameamuwa  kupita maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwapatia elimu wananchi hao katika kumiliki Ardhi kisheria na kupiga vita aina zote za udhalilishaji zilizopo katika shehiya zao.
Mawakili hao wamesema kutokana  na sheria zilizowekwa  katika Mahkama hiyo Mtu yeyote atakae miliki Ardhi ni vyema kujisajili ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima ndani ya Serikali na jamii kwa ujumla.
Hamisa Mmanga Makame mmoja ya Mawakili alisema wamechoshwa na vitendo vya udhalilishaji wanavyovisikia siku hadi siku vikiendelea ndani ya jamii jambo ambalo linalowaumiza vichwa katika utekelezaji wamajukumu yao.
Alisema licha ya Vitendo hivyo kuripotiwa siku hadi siku lakini wananchi walio wengi bado hawajawa na utayari wa kwenda kutoa ushahidi mahakamani kama inavyotakiwa.
“Utafiti ulibainisha ya kwamba Sheria iliyofutwa ilikuwa na mapungufu kadhaa ambayo bila ya kuondolewa udhalilishaji wa kijinsia ungelibakia kupigiwa kelele za bure na utekelezaji wa haki katika Mahakama za Kadhi ungeendelea kusuwasuwa” Alisema Wakili huyo.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na Watoto wao na kufuatilia nyenendo zao ili kuondokana na matatizo yanayowakabili  watoto hao.
Kwa upande wa Wananchi hao, wamewashukuru Mawakili hao kwa kuweza kufika Kijijini kwao na kutoa elimu stahiki katika wakati muafaka.
Wamesema elimu iliyotolewa wameipokea vyema na kuahidi kuwa wataifanyia kazi ipasavyo kwa lengo la kukomesha vitendo vya udhalilishaji katika jamii na migogoro ya ardhi.
Aidha Wananchi hao walisisitiza kuwa utaratibu ulioanzishwa wa kutoa Elimu hiyo ni vyema kuendelea kila mwezi ili kukabiliana vyema na matukio ya udhalilishaji na migogoro ya ardhi.
Mawakili hao wanaendelea na zoezi la utoaji wa elimu katika maeneo mbalimbali ya Vijijini ikiwa ni shamra shamra za maazimisho ya wiki ya sheria Zanzibar ambayo kilele chake ni Februari 12.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.