Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ajumuika na Wananchi Jiji la Dar es Salaam katika Kutoa Heshima za Mwisho Kwa Mzee Kingunge


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa wakihudhuria mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe Tanzania Mzee Kingunge aliyefariki juzi na kuzikwa leo Jijini Dar es Salaam. wakitowa heshima zao za mwisho wakati wa kuuanga mwili wa marehemu katika viwanja vya karimjee leo. 

Rais Mastaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho
Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akitowa heshima za mwisho baada ya kusaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho
Rais Mstaaf wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanasiasa mkongwe na kiongozi wa muda mrefu marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole mtoto wa kiume wa marehemu Kingunge anayefahamika kwa jina la Kinjekitile mara baada ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.