Habari za Punde

Wananchi Shehia ya Furaha washiriki ujenzi wa jengo la skuli ya Msingi Furaha, Chake Pemba

 WANANCHI wa Furaha wakibeba kokoto kwa ajili ya umwagaji wa zege katika banda moja lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi, ili wananfunzi waliohamishwa katika skuli ya Mabaoni waweze kurudi skulini kwao.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANANCHI wa Fura Wilaya ya Chake Chake, wakiponda zege kwa lengo al kwenda kumwaga katika madarasa manne mpya yanayojengwa na Baraza la Mji Chake Chake, kwa ajili ya wanafunzi wa skuli wa skuli hiyo, ambao kwa sasa wanasoma mabaoni.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 BANDA la vyumba vinne vya kusomea wananfunzi wa skuli ya Msingi Furaha Wilaya ya Chake Chake, likiwa katika hatua za mwisho kumalizika kwa ujenzi wake, banda hilo linalojengwa na baraza la mji chake chake linatarajiw akugharimu Milioni 20.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANANCHI wa Shehia ya Furaha Wilaya ya Chake Chake, wakiweka sawa fusi ndani ya moja ya banda la wanafunzi, ili kuweza kumwagwa kwa zege katika skuli hiyo.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MWENYEKITI wa Baraza la Mji Chake Chake, Sadik Omar Kassim mwenye koti jeusi, akimkabidhi mifuko 150 ya saruji Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Maafa katika skuli ya Furaha Kassim Khamis, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na baraza la Mji Chake Chake.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MAFUNDI Ujenzi katika shehia ya Furaha, wakimwaga zege na wengine kutandaza zege, katika moja ya mabanda ya skuli ya msingi Furaha Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyoweka na baraza la mji chake chake la kujenga skuli hiyo.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MWENYEKITI wa Baraza la Mji Chake Chake, Sadik Omar Kassim mwenye koti jeusi, akibeba zege kwenye bero kwa lengo la kumwaga katika moja ya madarasa ya skuli ya msingi Furaha.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
BAADHI ya magari ya abiria zenye rudi Chake-Uwanja wa ndege, zikiwa zimetulia katika skuli ya Msingi Furahaa, kufuatia siku maalumu kwa wananchi wote kushiriki katika zoezi la utiaji wa zege kwa skuli hiyo.(POCHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.