Habari za Punde

Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Yawakaribisha Wageni Wao Timu ya Wazee Arusha Sports Club Zanzibar Katika Michezo ya Pasaka Kesho Uwanja wa Amaan

Mwenyekiti wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Mhe. Hamza Hassan, akizungumza na kuwakaribisha Wageni wao wakati wa chakula maalum cha mchana kwa ajili ya kuwakaribisha na kumkaribisha Mgeni Rasmin Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma,kuzungumza na Wanamichezo wa Timu ya Wazee wa Arusha Sports Club. 
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma akizungumza na Wanamichezo wa Timu ya Wazee ya Arusha Sports Club, wakati wa kuwakaribisha na kujumuika katika chakula cha mchana baada ya kuwasili Zanzibar kwa ajili ya Tamasha la Michezo ya Pasaka. Kitaifa yanafanyika Jijini Dar es Salaam. Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club wenyeji wa Wazee Arusha Sports Club hubadilishana na kutembeleana kila mwaka katika maadhimisho ya Michezo ya Tamasha la Pasaka.
Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Wazee Arusha Sports Club Dr. Lawrences Nichael Mrema akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makaribisho na wenyeji wao Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Zanzibar, katika chakula maalum cha mchana kilichofanyika katika mghawa wa Baraza Chukwani Zanzibar. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika hafla na wageni wao wakati wa kutambulishwa na kuwakaribisha wageni wao. 
Wachezaji wa Timu ya Wazee Arusha Sports Club wakifuatilia mkutano huo wa makaribisho na wenyeji wao Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Zanzibar.


Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma akijumuina na Wageni wao Timu ya Wazee Arusha Sports Club katika chakula maalum waliowaandalia katika ukumbi wa mghawa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Makamu Mwenyekiti wa Wazee Arusha Sports Clum Dr, Lawrences Michael Mrema akijumuika katika chakula maalum walioandaliwa na wenyeji wao Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Zanzibar.  


Katibu wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Amour Mohammed akitowa neno la shukrani na kutowa utaratibu wa ratiba ya michezo ya Tamasha la Pasaka kwa Wageni wao Timu ya Arusha Sports Club baada ya kumaliza hafla ya chakula cha mchana. kilichofanyika katika mghawa wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.