Habari za Punde

Mawakala wa Tigo Pesa Wajinyakulia Mamilioni
Robert Butambele (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Sinza, Dar es salaam akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni kumi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Butembele  aliibuka mshindi wa kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia),   Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge. 
Said Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini, Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia),   Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.

Baadhi ya mawakala mbali mbali walioshinda zawadi katika promosheni ya mawakala wa Tigo pesa iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo. Hii ilikuwa baada ya kupokea zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. 

Wakala wawili (2) washinda TZS 10 millioni na TZS 5 millioni kila mmoja.


Nane (8) wapata TZS 3 millioni na TZS 2 millioni kila mmoja, huku mamia wengine wakizoa zawadi na bonasi lukuki


Dar es Salaam, 14 Machi, 2018.  


Kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.


Wakala RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo.  ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.


Pamoja na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.


Mojelwa Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya  Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara.  ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema kuwa lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni kuwadhamini na kuwashukuru mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini.


“Ningependa kuwapongeza mawakala wetu kwa kazi kubw wanayofanya ya kuhakikisha kuwa huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’ alisema.


Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.


Kampuni ya Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini.  Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.

Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.