Habari za Punde

Rais Dk Shein awaapisha viongozi aliowateua karibuni Ikulu leo

Baadhi ya Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliwaapisha Viongozi hao Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,[Picha na Ikulu,]28/03/2018.  

 Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kiapo cha Viongozi Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,walioapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu,] 28/03/2018. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali Iddi kabla kuwaapisha  Viongozi aliowateuwa hivi karibuni hafla hiyo ya kiapo ilifanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu,] 28/03/2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto katika hafla  iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu,] 28/03/2018.  

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika  hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu,] 28/03/2018.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                       28.03.2018
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.

Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Katika maelezo yao viongozi hao mara baada ya kuapishwa waliahidi kutekeleza majukumu yao kwa mashirikiano ya pamoja kati yao na viongozi wengine wote wa Serikali wakiwemo wale wa Wizara zao pamoja na Ofisi watakazoziongoza.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.