Habari za Punde

TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELEO.

Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA) mwezi huu imeandaa mkutano wa wanachama wake pamoja na wafanyabiashara kwa ujumla. Mkutano huu ambao umebatizwa jiina la TCCIA breakfast utajadili mambo kadhaa ikiwemo; Urahisishaji wa biashara za kimataifa kupitia Benki, Fursa zitokanazo na makubaliano kati ya TCCIA na Chemba ya China, Fursa katika biashara ya bomba la mafuta na pia uboreshaji wa mazingira ya biashara.
Akizungumzia mkutano huo Afisa Mkuu wa TCCIA Gotfrid Muganda alisema " huu ni mwendelezo wa ujengaji uwezo na kuwapa fursa wanachama wake na wafanyabiashara wa Tanzania". Pia TCCIA inalenga kurahisisha ufanyaji wa biashara kati ya China na Tanzania unaolenga kuondoa kabisa utapeli ambao baadhi ya wafanyabiashara wanakumbana nao. Mwaka jana TCCIA ilifanya mikutano kama hiyo mingi kwa mafanikio. Pia Leo hii Afisa Mtendaji Mkuu wa TCCIA Ndugu Muganda alikutana na mwambata wa ubalozi wa Algeria Nchini Tanzania na kuzungumzia ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria. Kupitia mkutano huo Ubalozi wa Algeria umetoa mwaliko wa maonyesho ya kibiashara Nchini Algeria yaitwayo Algeria International Fair mwezi wa tano Mwaka 2018. Mkutano wa breakfast umedhaminiwa na Azania Bank, Air Tanzania na Zurich Insurance

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.