Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Huawei unaoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Bw.Gao Mengdong (wa pili kulia) ujumbe huo ulipofika Ikulu Zanzibar leo kwa mazungumzo. [Picha na Ikulu.]
Rais Dk. Shein
alifanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya HUAWEI kutoka China
chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Kampuni hiyo tawi la Tanzania Gao Mengdong, Ikulu mjini Zanzibar.
Dk. Shein aliipongeza Kampuni
ya HUAWEI kwa kuendeleza mawasiliano ya kisasa kwa kuanzisha simu zenye mfumo
wa kisasa wa 5G pamoja na kueleza maendeleo ya miradi yao kwa Zanzibar pamoja
na mchakato wa mradi wa umeme wa kutumia jua.
Nao uongozi huo wa
HUAWEI ulimuahidi kuwa Kampuni yao iko tayari kushirikiana na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasilaino
pamoja na kuutumia uzoefu wake wa miradi ya umeme wa kutumia jua.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment