Na Said Abdulrahman Pemba.
WANACHAMA wa jumuia ya Umoja
wa Vijana wa CCM Wilaya ya Wete. wametakiwa kujikusanya pamoja na kuanzisha
vikundi vya ushirika katika matawi yao na kuacha kutegemea ajira Serikalini.
Akizungumza
na wanachama hao katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Wete,Katibu hamasa
kutoka Wilaya ya Kati Unguja, Ali Khamis Suleiman, alisema Serikali ulimwenguni
kote hazina uwezo wa kuajiri raia wake wote isipokuwa hufatafutia mbinu mbali
mbali za kujiajiri.
Alifahamisha
kuwa tatizo kubwa ambalo lipo katika visiwa hivi ni ukosefu wa ubunifu wa miradi ya maendeleo ila ajira zipo
nyingi tu wafanyakazi wa kazi hizo hawapo.
Alieleza
kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa hili na ndio maana Serikali zote mbili
zikawa zinatoa fursa kwa vijana wake.
“Sisi
vijana ndio wakuleta maendeleo katika taifa hili,na kama sisi tutaamua kufanya vitendo
vinavyoweza kuharibu amani ni sisi,”alisema Katibu huyo.
Sambamba
na hayo Katibu Ali, aliwataka wanachama hao kuachana na ile CCM ya zamani ya
iyena iyena tu bali ni kufanya kazi kwa uzalendo na kusimamia vyema ilani ya
Chama hicho.
Aidha
waliwataka wanachama hao kukitetea Chama chao na kutoa hoja pale ambapo itabidi
na kuwaeleza kuwa wasifanye makosa ambayo walifanya katika uchaguzi wa mwaka
2015.
Nao
baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walieleza
kuwa tatizo kubwa ambalo lipo katika maeneo yao ni kutokuwa na mashirikiano na
masheha wa shehia zao kwani wamekuwa wakiwadharau na kutowajali.
Aliutaka
uongozi wa Umoja huo kukaa pamoja na Masheha wote wa Shehia zilizomo ndani ya
Wilaya ya Wete ili kuwapa darasa ambalo litaweza kuondosha lawama juu yao.
“Licha
ya yote hayo ila pingamizi kubwa ambayo tunakabiliana nayo wakati tukiwa na
matatizo yetu ni masheha kwani tunapowaendelea na shida zetu wanatuambia sisi
hawatufahamu,”walisema wajumbe hao.
Hivyo
walisema wamepokea ujumbe huo na wako tayari kukaa pamoja na kujikusanya kwa
lengo la kufanyakazi za kujiletea maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment