Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Amali Nd. Salim Kitwana Sururu akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waajiriwa
wapya (walimu) Katika Ukumbi wa Baraza la Mji Chachani Chake Chake Pemba tarehe
24-25/03/2018
Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya
Raisi Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala bora Ndugu Massoud Ali Moh’d
akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waajiriwa wapya (walimu) Katika Ukumbi wa
Baraza la Mji Chachani Chake Chake tarehe Pemba 24-25/03/2018
Mratibu wa Taasisis ya Elimu Bi Asha Soud
Nassor akiwasilisha mada kuhusu mitaala katika mafunzo ya siku mbili kwa
waajiriwa wapya (walimu) Katika Ukumbi wa Baraza la Mji Chachani Chake Chake
Pemba tarehe 24-25/03/2018
Mrajisi Bi Hidaya Omar Khamis akiwasilisha
mada kuhusu miiko na maadili ya Ualimu katika mafunzo ya siku mbili kwa
waajiriwa wapya (walimu) Katika Ukumbi wa Baraza la Mji Chachani Chake Chake
Pemba tarehe 24-25/03/2018
Washiriki wa mafunzo (walimu) wakiwa katika
Ukumbi wa Baraza la Mji Chachani Chake Chake Pemba.
Na Ali Othman Ali, Pemba
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Amali Mh. Salim Kitwana Sururu amewataka wakaguzi kuwafuatilia kwa karibu
walimu walioajiriwa hivi karibuni ili kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa
ufanisi.
Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa walimu
82 waliojiriwa hivi karibuni katika ukumbi wa baraza la mji Chachani Chake
Chake Pemba, Mh. Sururu amewataka walimu hao kulinda heshima na kujipatia
umaarufu kwa kufundisha kwa bidii na kujifunza zaidi.
Kwa upande wake Mratibu wa Taasisis ya
Elimu Bi Asha Soud Nassor akiwasilisha mada kuhusu mitaala aliwataka walimu
kufundisha kwa kutumia vifaa na teknolojia badala ya kutumia kitabu cha
mwanafunzi pekee.
Kwa upande wake Mrajisi Bi Hidaya Omar
Khamis ameawataka walimu hao kuielewa sharia ya elimu namba 6 ya mwaka 1982,
kanuni za miiko na maadili ya kazi ya ualimu chini ya kifungu cha 59 (1) (Z).
Akifafanua kanuni hiyo Bihidaya amesema Mtu
yeyote anaetaka kuajiriwa katika kazi ya ualimu atalazimika kuliridhisha baraza
la elimu kwamba pamoja na sifa za kielimu anao mwelekeo wa kua mwalimu
muadilifu.
Bi Hidaya ameongeza kwamba niwajibu kwa kila
mwalimu kufuata miiko ya ualimu wakati wote akiwa ndani na nje ya skuli.
Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya
Raisi Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala bora Ndugu Massoud Ali Moh’d akifunga
mafunzo hayo amewataka walimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia sharia na kanuni
za Utumishi wa Umma na kuacha mambo yote yanayokwenda kinyume na sharia hiyo.
Nd. Masoud amewasihi walimu hao kutambua
nafasi yao kama watumishi wa umma hivyo hawana budi kutii serikali na viongozi
waliopo madarakani ikiwa ni moja ya kanuni katika sharia ya Utumishi.
“Sharti jengine kwa mujibu wa kanuni hii
nilazima mtumishi wa umma aheshimu viongozi na Serikali iliokuwepo madarakani,
mkono unaokulisha usiutemee mate” Alisisitiza Nd. Moh’d.
Jumla ya walimu 82 walioshiriki mafunzo
hayo wameshaanza kazi katika skuli mbali mbali kisiwani Pemba na kupunguza
tatizo la uhaba wa walimu katika skuli za serikali.
No comments:
Post a Comment