Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yafanya Mkutano Mkuu wa Mapitio ya Mkakati Mkuu wa Afya.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Mpango mkakati wa tatu wa Afya kwa kipindi cha miaka mitatu uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View mjini Zanzibar.
Mwakilishi mkaazi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu duniani nchini Tanzania UNFPA Jaquline Mahon akiwasilisha salamu zake kwa niaba ya Mashirika ya Umoja wa mataifa katika hafla ya uzinduzi wa Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Mpango mkakati wa tatu wa Afya kwa kipindi cha miaka mitatu uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdulla akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kufungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Mpango mkakati wa tatu wa Afya kwa kipindi cha miaka mitatu uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia uwasilishwaji wa taarifa.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na Mwakilishi mkaazi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu duniani nchini Tanzania UNFPA Jaquline Mahon wakiwa katika picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Mpango mkakati wa tatu wa Afya kwa kipindi cha miaka mitatu uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View mjini Zanzibar.
Na.Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar. 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuifanyia mabadiliko Sekta ya Afya kwa lengo la kuziimarisha afya za Wananchi hususan wanawake, watoto na makundi maalum.
Mchakato wa mabadiliko unahusisha kuzishirikisha sekta mbali mbali kwa madhumuni ya kuziimarisha afya za Wananchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed wakati akifungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Mpango mkakati wa tatu wa Afya kwa kipindi cha miaka mitatu uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View mjini Zanzibar.
Amesema lengo la kuwasilisha ripoti hiyo ni kutoa fursa kwa Washiriki kuielewa na kutoa michango yao ambayo itaimarisha afya za wananchi wa Zanzibar.
Waziri Hamad amefahamisha kuwa toka kuanzia miaka ya 1990 Wizara ya Afya imetekeleza mipango mikakati mitatu ambayo imesaidia kufanya tathmini na uchambuzi wa utekelezaji kwa kipindi chote hicho.
Aidha aliyashukuru sana Mashirika ya Umoja wa mataifa kwa mashirikiano makubwa ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika Wizara ya Afya.   
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Asha Abdulla wakati akimkaribisha Waziri guyo amesema zoezi la kuandaa Ripoti hiyo lilifanywa na Wizara kupitia Idara ya Mipango, Sera na Utafiti kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo WHO, UNFPA na UNICEF.
Akielezea malengo yaliyofanikiwa katika Ripoti hiyo amesema ni pamoja na kupambana na Ugonjwa wa Malari na maambukizi ya Virusi vya ukimwi ambapo magonjwa yote hayo kwa sasa yapo chini ya asilimia moja.
Eneo jingine ambalo limefankiwa ni kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano na Watoto wachanga na kusema kuwa juhudi zinapaswa kuendelezwa zaidi katika kudhibiti vifo hivyo.
Akielezea changamoto ambazo zimejitokeza katika Ripoti hiyo amesema ni pamoja na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo Saratani, Sukari na Moyo ambapo kwa sasa Serikali imeanza kuchukua hatua za kukabili maradhi hayo.
Miongoni mwa hatua zilizochukua ni pamoja na kuanzishwa Kliniki ya Sratani na Kliniki ya kusafisha Maradhi ya Figo katika Hospital ya Mnazi mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.