Habari za Punde

Taarifa ya mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kuhusu kutofuata sheria barabarani




Katika kukabiliana na ongezeko la ajali zisizo za lazima , zinazo sababishwa na madereva wasiofuata sheria na nyengine kwa uzembe, nimemuagiza kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba kuwakamata wote wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuzingatia sheria za barabarani ikiwamo mwendo kasi nyakati za usiku na kuwapeleka mahakamabi.

Tokea zoezi hili lianze jana zaidi ya vyombo 100 vimekamatwa  kwenye operesheni  hiyo.

Lengo letu ni   kudumisha nidhamu barabarani  ili kupunguza ajali zisizo hizo  na kwasasa kazi hii ya ukamataji kwa wasio tii sheria itakua endelevu kwa muda wote mchana na usiku wake.

Tukinge ajali kuliko kutibu,  inawezekana mkataze mtoto wako  asivunje sheria la si hivyo ataingia mikononi mwa jeshi letu, tuweke nidhamu ya utembeaji barabarani pamoja na kufuata sheria zote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.