Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya shamba la mpunga katika bonde la Kizimbani toka kwa Katibu wa Jumuiya ya Wakulima Kizimbani Bw. Shafii Kibwana Said ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuweka kaa kwenye maji kama ishara ya kuhamasisha utunzaji mazingira na uzalishaji wa katika eneo la Fuoni Kibondeni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kibondeni mara baada ya kuweka jiwe la ujenzi wa Tawi hilo mkoa wa Mjini Magharibi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais ameahidi
kuwapatia trekta moja wakulima wa mkoa wa Mjini Magharibi ili liweze kusaidia
wakulima kulima kwa wakati.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
leo wakati alipotembelea Mradi wa Wakulima wa Mpunga katika bonde la Kizimbani
liliopo wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais aliwaambia
wakulima hao kuwa Mjenga Nchi ni
Mwanachi na aliwahimiza viongozi wote kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli
za kuleta maendeleo na kushirikiana bega kwa bega na wananchi.
Makamu wa Rais ambaye
ameanza ziara ya siku nne ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya CCM Zanzibar,
amewataka viongozi na wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kushirikiana na
kudumisha amani ya nchi.
Pamoja na kutembelea shamba
la mpunga ambapo alisimamia zoezi la upandaji mpunga Mheshimiwa Makamu wa Rais
alitembelea eneo la Fuoni Kibaoni ambao alishuhudia upandwaji wa miti ya mikoko
kwa kiasi kikubwa ikiwa shemu ya utunzaji wa mazingira lakini pia utunzaji na
uzalishaji wa Kaa.
Katika ziara hiyo Makamu wa
Rais aliambata na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi,
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na Viongozi wengine wa Chama na
Serikali.
No comments:
Post a Comment