Habari za Punde

TANZANIA YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI KUBORESHA BARABARA YA UVINZA-MALAGARASI KWA KIWANGO CHA LAMI

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akisalimiana na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, alipowasili Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi, kwa ajili ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (wa tatu kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami. kulia kwake ni Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk na Mkuu wa Dawati la Abu Dhabi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Kuchaka.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), akisindikizwa na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, baada ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakibadilishana mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto),  na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakionesha mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
​Na.Benny Mwaipaja, Abu Dhabi
Tanzania imeendelea kuaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ambapo Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Falme za Kiarabu-Abu Dhabi, umeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 15, sawa na shilingi bilioni 34 za Tanzania, kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami
Hafla fupi ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya Mfuko huo yaliyopo Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, amesaini kwa niaba ya Serikali, na Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa niaba ya Mfuko huo.
Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, Katibu Mkuu-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa ni kiungo kikuu cha usafiri wa abiria na mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigoma na nchi jirani za Burundi na Kongo DRC.
Amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuboresha barabara hiyo kwa kiwango cha lami umelenga kuchochea uchumi wa nchi kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao ya wakulima pamoja na kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kufanya biashara na nchi hizo jirani.
"Tutabakiwa na kipande cha barabara yenye urefu wa kilometa 28 kutoka Urambo hadi Kaliua na kilometa 42 kutoka Chagu hadi Kazilambwa, barabara ambazo Serikali inaendelea kuzitafutia fedha ili kukamilisha barabara yote inayoelekea ukanda huo wa kati kutokea Dar es Salaam, Manyoni (Singida), Tabora hadi Kigoma" Alisema Mhandisi Iyombe.
Ameushukuru Mfuko huo kwa kuendelea kuiamini Serikali na kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu baada ya kufanya hivyo hivi karibuni kwa kutoa mkopo mwingine wa dola milioni 57, uliofanikisha kuboreshwa kwa barabara ya Kidahwe hadi Uvinza yenye urefu wa kilometa 77 kwa kiwango cha lami.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi, kwa upande wake, amesema kuwa Mfuko huo uko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Amefafanua kuwa mradi huo ambao mkataba umesainiwa mjini Abu Dhabi, utakuwa ni wa nne kufadhiliwa na Mfuko wake Tangu uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Tanzania uanzishwe mwaka 1977, ukiwemo mradi wa kuendeleza kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mradi wa Maji Vijijini huko Viwani Zanzibar na Mradi wa kuboresha barabara ya Kidahwe hadi Uvinza kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk  amesema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni kiashiria cha kukubalika kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya haraka na kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.
"Hatua hii ni uthibitisho wa mahuasiano mazuri ya kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1977" Alisisitiza Mhe.Mbarouk
Mhe. Mbarouk amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ya Uvinza hadi Malagarasi kutachochea maendeleo ya kiuchumi na mapinduzi ya viwanda kwa kuunganisha shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na maliasili pamoja na kukuza utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.