Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Apokea Ndege Mpya ya Bombardier Q400 Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku ikipewa heshma ya  kumwagiwa maji(water salute) mara baada ya kutua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, pamoja na viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa Serikali wakipiga makofi wakati wakiipokea Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwa imeegeshwa  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono marubani wawili waliokuja na ndege hiyo mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono na kushukuru  wakati akiingia katika ndege hiyo mpya ya Bombardier Q400 iliyowasili kutoka nchini Canada
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa dini na wa ATC ndani ya ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400  ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye  ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400  ilipoipokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka  huku akishuhudiwa na marubani mara baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400  ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishangiliwa na umati wa wananchi baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipongezwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya KKKT Dkt.  Alex Malasusa baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga  baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, leo Aprili 2, 2018..(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.