ENEO Changaweni la barabara ya Mkoani-
Chake chake Pemba, ambalo limeharibika tena kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha, ambapo mwezi Mei mwaka jana, pia eneo liliharibika na kujengwa bila
ya mafanikio, ambapo kwa sasa wizara ya ujenzi Pemba, imerejea kuitengeneza
kipande cha barabara yake za zamani, na ndio wananchi wanapotumia kwa sasa, (Picha na Haji Nassor).
FOLENI ya gari baadhi yao zilizobebea mizigo ya abiria
walioshuka meli wakitokea Unguja, ambapo walilazimika kukaa eneo la Changaweni Mkoani
kwa saa mbili, kufuatia barabara kuharibika na eneo lililoruhusiwa kupita kwa
dharura, nayo gari ya mzigo inayodaiwa ni ya Kampuni ya Azam kukwama, (Picha na Haji Nassor).
MOJA ya gari za abiria aina ya Dyna,
inayofanya kazi zake Mkoani-Chakechake, ikivutwa na gari la kijiko, baada ya
kukwama eneo ambalo pia gari ya mzigo inayodaiwa kuwa ni ya Kampuni ya Azam,
kukwama na kusababisha foleni, iliodumu kwa saa mbili, eneo la Changaweni
Mkoani, ambapo barabara ya kawaida iliharibi kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha, (Picha na Haji Nassor).
GARI ya mzigo inayodaiwa kuwa ni kampuni ya Azam,
ikiwa imeshatolewa na gari la kijiko, ambapo gari hiyo ilikwama eneo la
barabara ya dharura hapo Changaweni Mkoani, na kusababisha, abiria waliokuwa
wakitokea Unguja na wengine Chake chake, kukwama kuanzia saa 10:00 jioni hadi
12:44, (Picha na Haji Nassor).
No comments:
Post a Comment