Habari za Punde

Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Aendelea na Ziara Yake na Kutembelea Baraza la Wawakilishi na Kuzungumza na Mhe. Spika wa Baraza Zuberi Ali Maulid.

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akisalimiana na Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr. Salim Mohammed , alipofika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mazungumzo na Spika na kuangalia shughuliza za Vikao vya Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati wa Ziara yake ya wiki moja Nchini Zanzibar. 
Waziri wa Habati Utali na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimtambulisha Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid kwa Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr. Salim Mohammed , alipofika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar akiwa katika ziara yake Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitzungumza wakati wa mkutano wa Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr.Salim Mohammed alipofika kuonana na Spika wa Bara za la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberia Ali Maulid Chukwani Zanzibar. 
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akizungumza na Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr. Salim Mohammed , alipofika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza zinavyoendeshwa , akiwa katika ziara yake Zanzibar

Katibu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr. Salim Mohammed, akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa mkutano wake na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid alipofika katika majengo ya Baraza Chukwani Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.