Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wajumbe Wakichangia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais MBLM.

Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Pemba Mhe. Shehe Hamad Mattar akiochangia Hutuba ya Bajeti ya Fedha ya Matumizi kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi linalofanyika katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Mawaziri wa Wizara mbali mbali wakifuatlilia michango ikiwasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar Mhe. Jaku Hashim Ayoub akisoma Kitabu cha Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na MBLM wakati wajumbe wakichangia hutuba hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe. Miraji Kwaza akichangia Hutuba ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na MBLW katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Waheshimiwa Mawazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kuwasilishwa Michango ya Wajumbe wa Baraza.
Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar Mhe. Jaku Hashim Ayoub akichangia Hutuba ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na MBLW.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan na Mhe. Ali Suleiman Shihata wakifurahia jambo wakati Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar akichangia katika Mkutano huo wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Mwakilishi wa kuchanguliwa kupitia Nafasi za Rais Mhe. Said Soud Said akichangia katika mkutano huo wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019, iliowasilishwa katika ukumbi wa mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na MBLW Mhe. Issa Haji Gavu akiandika michango wakati wa kuchangia Hutuba yake ya Bajeti ya fedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Wakati wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakichangia.

Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mhe Mwanaasha akitoka katika ukumbi wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na MBLW na kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana. wakiwa nje ya ukumbi baada ya kuahirishwa wakibadilishana mawazo baada ya kuipitisha Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na MBLW.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakibadilishana mawazo baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa Baraza kwa mapumziko ya mchana.
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe. Haroun Ali Suleiman akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Mhe. Abdallah Maulid Diwani wakiwa nje ya ukumbi wa mikutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.


WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani wakibadilishana mawazo kushoto Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil na kulia Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Hassan Khamis Hafidh wakibadilishana mawazo baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , kwa mapumziko ya mchana

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.