Habari za Punde

Harusi ya Kifalme ya Prince Harry na Meghan Markle: Mwanamfalme Harry na Meghan wafunganishwa katika ndoa Windsor Castle

Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.
 Mwanamfalme Harry na msimamizi wake kwenye harusi, kakake Mwanamfalme William
Meghan na Harry wakitangazwa kuwa Mume na Mke

 Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.
Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.
Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.
George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.

Mwanamfalme Harry na Meghan Markle katika kanisa la St George, Windsor Castle
 Wawili hao wakiwa wameketi kanisani
 Mwanamfalme Charles (babake Prince Harry) akimsindikiza Bi Markle kumpeleka kwenye madhabahu

Mamake Meghan, Doria Ragland, ndiye jamaa pekee wa Bi Markle aliyehudhuria sherehe hiyo
 Oprah Winfrey (mwenye vazi la waridi) na mwigizaji Idris Elba wakiwasili kwa sherehe


 Baadhi ya waliofika kutazama harusi hiyo wamevalia mahsusi. 
Janet Butterfield na Ray Brown kutoka Bradford, Yorkshire wanasema harusi ya sasa inavutia zaidi kuliko ya Mwanamfalme William na Kate
Wengi walifika Windsor kushuhudia harusi wa Mwana Mfalme leo jumamosi. 
Grace Gothard kutoka London aelezea furaha yake kuhudhuria harusi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.