Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha AFP Mhe. Said Soud Ampongeza Msajili wa Vyama Vya Siasa Tanzania.


Na. Bakari Mussa -Pemba.
Chama cha Siasa cha Alliance for Farmers Party Tanzania (AFP),kimempongeza Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania , Jaji Francis Mutungi, kwa kusimamia vyema Demokrasia ndani ya mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini .

Kiongozi huyo, ameonesha uadilifu wa kuvilea na kuvisimamia Vyama hivyo sambamba  na kuchukuwa juhudi za maksudi ili kuona Siasa za nchi zinaimaika na kufanya vizuri kwa mujibu wa Sheria za nchini.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi , Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Mhe.Said Soud Said, alisema Msajili wa Vyama amekuwa ni mlezi pia katika baraza la Vyama  vya siasa,na kuvifanya vyama hivyo viweze kuondosha tafauti zao za kisiasa katika kujenga Tanzania mpya.

Alifahamisha ndani ya Baraza hilo la Vyama vya Siasa kumekuwa na mambo mengi yanayo isaidia Serikali katika kufikia Demokrasia ya kweli na sasa ni   wakati  muafaka kwa Msajili kuchukuwa hatuwa za kuelimisha Demokrasia kwa kuruhusu Baraza hilo kufanya semina za mara kwa mara  ambazo zitawafanya viongozi wa vyama kuelekeza nchi pale inapotakiwa.

Soud, alieleza Vyama vya Siasa Tanzania ni vyama ambavyo vinahitaji kupigiwa mfano katika kuendeleza Siasa ya amani na utulivu ambayo kwa sasa  ni mfano wa kuigwa barani Afrika na Duniani kote.

‘’ Ni vizuri baraza la  Vyama vya Siasa kuendelea kukutana mara kwa mara ili kuondosha ile dhana iliojengeka kwa baadhi ya Vyama, kuona Demokrasia imebanwa ukweli ni kwamba iwapo   Baraza hilo litaendelea kukutana mara kwa mara hali kama hiyo haitoweza kujitokeza tena,na pia  itampa nguvu Msajili wa Vyama kuelewa ya moyoni walionayo Viongozi wa vyama hivyo katika nchi yao,’’ alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema ni jambo la busara kwa baraza hilo kuendelea kukutana kama ambavyo sasa hivi Mwenyekiti wa baraza hilo.Mhe.Shibuda yumo katika mchakato wa kuvitaka vyama hivyo vikutane mara kwa mara, hivyo ni wajibu wa Viongozi wa Vyama kumuunga mkono ili kuweza kupata nafasi hiyo kwenye Serikali ili  Vyama viweze kuondosha ile tafauti zao
ndani ya kujenga Demokrasia ya Tanzania .

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania , anafaaa kuchukuwa juhudi katika kushirikiana na masajili kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya Tanzania.

Aidha Chama cha AFP, kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk, Ali Mohamed Shein, kwa kusimamia vyema suala la amani na Utulivu  ndani ya Jamhuri ya Muungano Tanzania .

Mwenyekiti huyo wa Chama cha AFP Taifa , Said Soud Said, alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ni mfamo wa kuigwa katika kusimamia na kulea  suala la amani na utulivu barani Afrika na Dunia kwa ujumla.

‘’Viongozi hawa wameweza kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya Viwanda jambo ambalo Wananchi waliowengi wanaendelea kuipenda nchi yao,’’, alieleza.

Kwa upande mwengine  Chama cha AFP, kinachukuwa fursa ya kuwashauri Wakulima kuzitumia mvua zinazonyesha kwa kuzitumia kwa ajili ya kupanda mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda na  biashara jambo ambalo linaweza kuwatowa katika umaskini.

Hata hivyo alisema pamoja na kwamba mvua hizo zimeleta maafa makubwa lakini sio za kuzidharau katika kuzifanyia kazi ya Kilimo, ambacho kinaweza kuwasaidia Wananchi hapo baadae

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.