Habari za Punde

Wakulima wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba Wafaidika na Zao Hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Kasikazini Pemba.Mhe.Omar Khamis Othman, akifunguwa mkutano wa Wakuliam wa Karafuu Wilaya ya Micheweni uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika Biashara la Taifa ZSTC Zanzibar,Ndg. Maalim Kassim Suleiman, akiwapongezaWakulia wa Zao la Karafuu wa Wilaya ya Micheweni kwa kuuza Karafuu kwa wingi katika vituo vya Shirika hilo na kuweza kuvuuka malengo yaliowekwa .
Mdhamini wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC ) Pemba,Ndg. Abdalla Ali Ussi, akieleza machache juu ya juhudi zilizochukuliwa na Wananchi wa kisiwa cha Pemba , katika kulisimamia na kuuza karafuu zao katika Vituo vya Shirika na kulifanya shirika hilo liweze kuvuuka malengo yake.
Baadhi wa Wakulima wa Zao la Karafuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba pamoja na Masheha wa Wilaya hiyo wakifuatilia kwa makini katika Mkutano wa ZSTC na Wakulima hao uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba.


Baadhi wa Wakulima wa Zao la Karafuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba pamoja na Masheha wa Wilaya hiyo wakifuatilia kwa makini katika Mkutano wa ZSTC na Wakulima hao uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba.(Picha na Jamila Abdallah -Maelezo Pemba)JUMLA ya Tshs BILION 119.4 , zimeingia katika mikononi  mwa  Wananchi baada ya Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) kununuwa Karafuu katika msimu  wa mwaka 2017/2018.

Fedha hizo zimetokana na Shirika hilo kununuwa Tani 8533.65 ya Karafuu kutoka kwa Wakulima wa Zao hilo Visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika Mkutano wa Wakulima wa zao la Karafuu katika Wilaya ya Micheweni , mkurugenzi fedha wa Shirika la ZSTC Zanzibar , Ismail Omar Bai ,  alisema msimu wa mwaka 2017/2018, Shirika lilitarajia kununuwa tani 6770 za Karafuu kutoka kwa Wakulima hao.

Alieleza kuwa  malengo ya Shirika ni kununuwa Tani 6770 ,lakini kiutoka na muitikio wa Wakulima kuuza Karafuu zao katika Shirika hilo limesababisha kuvuuka malengo .

‘’ Tunatowa pongezi kwa Wakulima wa Zao hilo kwa juhudi zao za kuuza Karafuu  zao kwenye Vituo vya Shirika , hivyo tunawaomba muongeze juhudi   zenu ili kuleta mafanikio makubwa kwa  Serikali na nyinyi binafsi,’’ alisema.

Mapema akifunguwa mkutano huo , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Omar Khamis Othman,alisema msimu huu Shirika limefanikiwa vizuri kwa kununuwa tani nyingi zaidi za Karafuu kuliko miaka mingine , jambo ambalo litaweza kuleta maendeleo zaidi katika nchi.

‘’ Ushirikiano uliokuwepo baina ya Serikali ya Mkoa , Shirika la ZSTC,pamoja na Wakulima katika kuhakikisha wakulima wanauza Karafuu zao kwenye vituo vya Shirika tunashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,’’, alifahamisha Mkuu wa mkoa.

Mkuu huyo wa Mkoa , aliwataka Wakulima hao kuongeza juhudi za kuendelea kuiuzia Karafuu zao Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) ili kujiletea maendeleo zaidi ya kiuchumi katika nchi.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka Shirika la ZSTC,  Maalim Kassim  Suleiman, alisema kuwa juhudi za wakulima pamoja na uaminifu wao wa kuuza Karafuu zao kwenye shirika hilo, ndio zilizoleta mafanikio makubwa kwa msimu huu.

Nae Mdhamini wa Shirika hilo, Abdalla Ali Ussi,alisema kuwa Wakulima wa Zao hilo  wameonesha uaminifu jambo ambalo limepelekea msimu huu kununuwa tani nyingi zaidi kuliko miaka 21 iliopita.

Akichangia mada katika mkutano huo , Sheha wa Shehia ya Micheweni Pemba, Dawa Juma Mshindo,aliliomba Shirika kuwapa Wakulima wa mikarafuu Miche bila ya ubaguzi,ili kuweza kuimarisha Kilimo hicho

Nae Mkulima wa kutoka katika shehia ya Konde , Khamis Cholo, alisema bado juhudi zinahitajika kuchukuliwa na taasisi husika ili kuliimarisha zao hilo la Karafuu.

‘’ Mimi kila nikienda kutaka Miche ya Mikarafuu , naambiwa Micheweni haimo ,sijuwi tatizo nini , hivyo naomba mutuangalie kwa jicho la imani na sisi tupate’’ alisema.

Mkutano huo wa wakulima kwa Wilaya ya Micheweni Pemba, umefanyika katika katika Skuli ya Sekondari Micheweni na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali mbali wa Serikali ya Mkoa na Wakulima wa Karafuu waliomo katika Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.