Habari za Punde

JUMIA FOOD TANZANIA YASHUSHA GHARAMA YA KUAGIZA CHAKULA KWA 95%




KATIKA jitihada za kutoa huduma nafuu ya chakula mtandaoni, Jumia Food imeshusha kiwango cha chini cha kuagiza chakula kupitia mtandao wake mpaka kufikia shilingi 500!

Kabla ya punguzo hilo, kiwango cha chini cha kuagiza chakula kilikuwa ni kati ya shilingi 7000 mpaka 10000, kutegemeana na utaratibu wa mgahawa pamoja na umbali alipo mteja. Maboresho haya yanalenga kuwapatia wateja machaguo mengi zaidi na unafuu kwa wateja kuweza kuagiza vyakula wavipendavyo kwa gharama ndogo.


Meneja Mkazi wa Jumia Food Tanzania, Xavier Gerniers amebainisha kuwa lengo kuu ni kufafanua zaidi juu ya dhana kwamba huduma ya chakula kupitia mtandaoni ni ghali na inawalenga watu wenye vipato vya juu.


“Kwa kufanya hivi, tunawahakikishia wateja wetu kwamba sasa wanaweza kuagiza na kufurahia chakula bila ya hofu ya bajeti waliyonayo,” alisema Gerniers na kuongezea kuwa kushuka kwa bei pia kutaiwezesha kampuni kugusa mahitaji na matakwa ya wateja tofauti.  


“Lakini cha muhimu zaidi, ni kuwahamasisha Watanzania kuchangamkia fursa ya huduma ya chakula kwa njia ya mtandao ili kurahisisha shughuli zao za kila siku. Unaweza kupata huduma ya chakula kutoka kwenye migahawa mbalimbali kupitia Jumia Food kwa kutumia simu yako ya mkononi na kufaidika na ofa hizi lukuki kutoka Jumia Food,” aliongezea Meneja Uhusiano wa Umma, Kijanga Geofrey.


Huduma za chakula kwa njia ya mtandaoni ni maarufu kwenye miji tofauti duniani kwa sababu husaidia kuokoa muda na gharama kwa wateja. Kwa kuongezea, huongeza thamani kwa wamiliki wa migahawa kupitia fursa ya bure ya kufanyiwa shughuli za kimasoko hivyo kujiongezea idadi ya wateja wa mtandaoni waliopo katika maeneo tofauti. Kwa upande mwingine, wateja nao hunufaika kwa kupata huduma ya chakula kutoka kwenye migahawa wanayoipenda bila ya kuitembelea moja kwa moja.


Mapema mwaka huu, Jumia Food ilizindua programu yake ya simu ya mkononi iliyofanyiwa maboresho zaidi. Kwa mfano, kupitia maboresho hayo mteja ana uwezo wa kupata orodha ya migahawa iliyo karibu yake yenye huduma ya chakula anachotaka kuagiza.


Kuhusu Jumia Food

Jumia Food Tanzania ni mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma ya chakula kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. Jumia Food ipo kwenye nchi 11 barani Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Morocco na Uganda. Huduma hii huwawezesha wateja kwa kupata huduma ndani ya wakati, huongeza wateja, kusaidia uendeshaji na njia za masoko.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.