Habari za Punde

Wafanyakazi wa Gazeti la Serikali la Zanzibar Leo Kisiwani Pemba Wajipongeza Kwa Ufanisi wa Utendaji Kazi Wao Kuwahabarisha Wananchi.

MDHAMINI wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar-Zanzibarleo Ofisi ya Pemba Bakari Mussa Juma, akisoma taarifa fupi ya shirika hilo la Magazeti ya Serikali Zanzibar, kikao hicho cha kujitathmini na kujipongeza kwa wafanyakazi wa shirika hilo, huko katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake.
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Pemba Ndg.Khatib Juma Mjaja, akizungumza na kufungua mkutano maalum wa tathmini na kujipongeza juu ya kazi za Shirika la Magazeti ya Serikali zanzibarleo kisiwani Pemba, kwa wadau wa shirika hilo huko katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake Pemba.
MWENYEKITI wa Pemba Press Club (PPC) Said Mohamed Ali, akitoa mchango wake katika kikao cha kujitathmini na Kujipongeza kwa wafanyakazi wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Zanzibarleo Pemba juu ya mabadiliko makubwa ya gazeti hilo kwa sasa
MRATIB wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akitoa neon la shukurani juu ya hutuba ya mgeni rasmi kwa waandishi wa habari wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, zanzibarleo ofisi ya Pemba huko katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake
MWANDISHI wa Habari mwandamizi wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar-Zanzibarleo Ofisi ya Pemba, Haji Nassor Mohamed akitoa shukurani kwa wadau mbali mbali wa habari, katika kikao cha kujitathmini na kujipongeza kwa wafanyakazi wa shirika hilo huko katika Ukumbi wa Tasaf Chake Chake
MENEJA wa Redio Jamii Mkoani Ali Abass Omar, akitoa nasaha zake kwa waandishi wa habari na wafanyakazi wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, zanzibarleo Ofisi ya Pemba katika kikao chake cha kujipongeza na kujitathmini kilichofanyika katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake

MRATIB wa Tasaf Chake Chake Pemba Mussa Said, akitoa nasaha zake kwa waandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Zanzibarleo Ofisi ya Pemba katika kikao cha Kujitathmini na Kujipongeza juu ya utendejai wao wa kazi, kikao kilichofanyika katika ukumbiwa Tasaf Chake Chake.
MSAIDIZI wa Makamu wa Pili wa Rais Pemba Amran Massoud Amran, akitoa ushauri kwa waandishi wa habari na wafanyakazi wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, zanzibarleo ofisi ya Pemba katika kikao chake cha kujitathmini na kujipongeza kilichofanyika katika ofisi ya Tasaf Chake Chake Pemba
WAANDISHI wa Habari na Wadau wa habari Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini mkutano wa Kujitathmini na kujipongeza kwa wafanyakazi wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, zanzibarleo Ofisi ya Pemba kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Tasaf Chake Chake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.