Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri Awasilisha Hutuba ya Bajeti ya Wizara Yake Kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Baraza la Wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ ikisomwa na Waziri husika Mhe. Haji Omar Kheri katika Mkutano wa kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.
Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Shehe Hamad Mattar akiongoza Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ikisomwa na Mhe. Haji Omar Kheri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala zav Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri akisoma Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2018/2019. Kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wakifuatilia hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Idara Maalum Zanzibar ikiwasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Haji Omar Kheri.

Viongozi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Wizara yao ya Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019. ikiwasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Haji Omar Kheri akiiwasilisha kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.