Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo Michango ya Bajeti ya Wizara ya Afya Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akichangia Hutuba ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar katika Mkutano wa Kumi Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar, akisisitiza jamba wakati akiwailisha mchango wake.

Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mwanaasha akifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati akiongoza Baraza la Wawakilishi katika kipindi cha Michango ya Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akisisitiza wakati wa kuchangia hutuba ya bajeti ya Wizara ya Afya akionesha Kadi ya Bima ya Afya itumike kwa Wananchi wa Zanzibar ili kupunguza gharama.
Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar Mhe. Ali Suleiman Shihata akichangia Hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya akisoma baadhi ya vifungu vya hutuba ya bajeti hiyo wakati akichangia  
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mhe. Mohammed Raza akichangia hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya kwa mwaka wa matumizi 2018/2019.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashi Mohammed akiwa na Naibu wake Mhe. Harusi Said, wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kipindi cha michango ikiendelea katika ukumbi wa mkutano wa Baraza Chukwani Zanzibar.  No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.