Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Azindua Mfumo wa Usajili Kwa Kutumia Mtandao wa Kumpyuta Kwa Taasisi za Biashara na Amana Kwa Mali Zinazohamishika Zanzibar.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili Biashara na Mali Zanzibar. Ndg. Abdallah Waziri, akitowa maelezo ya kitaalamu jinsi ya Usaji wa Biashara na Amana Zanzibar wakati wa Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idirisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na Kuzinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa Kutumia Kompyuta kwa Taasisi za Biashara na Amana kwa Mali Zinazohamishika, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Juma Ali, akizungumza wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali kuhutubia na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kufanya Uzindu huo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akihutubia wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kutowa nasaha zake na kufanya Uzinduzi huo wa Usajili ya Mfumo wa Biashara na Amana na Mali Zisizohamishika.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.