Habari za Punde

Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Waangamiza ZFDA Waangamiza Tani 20 za Maziwa Yalioharibika.

Wafanyakazi wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) wakiteremsha Maziwa yalioharibika kwenye gari kwa ajili ya kuyaangamiza katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kuangamiza bidhaa zilizokwesha muda wake na kutofaa kutumika kwa matumizi ya Binaadame eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Wafanyakazi wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) wakiteremsha Maziwa yalioharibika kwenye gari kwa ajili ya kuyaangamiza katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kuangamiza bidhaa zilizokwesha muda wake na kutofaa kutumika kwa matumizi ya Binaadame eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.Mkoa wa Kusini Zanzibar.
 GARI aina ya Katapila likisaga maziwa yalioharibika na yasiyofaa kwa matumizi ya Binaadamu  katika zoezi lililofanyika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja. 
KAIMU Mkurugenzi ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungumzia zoezi la Uteketazaji wa Maziwa tani 20 yalioharibika katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.
Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imewakumbusha Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za Chakula kutoka nje kuhakikisha wanafuata miongozo, sheria na kanuni za usafirishaji ili kuhakikisha bidhaa zao zinafika nchini zikiwa salama kwa matumizi ya wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali Omar alisema hayo katika Jaa la Kibele kwenye zoezi la kuteketeza maziwa yaliyoharibika kwa kusafirishwa kwenye kontena moja na mizigo mengine ikiwemo gari kutoka Dubai.
Alisema baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka kutokana na msukosuka wa meli baharini na kuharibu maboksi mengine yaliyopelekea maziwa yote yakose sifa ya matumizi ya binadamu.
Aliwashauri wafanyabiashara kuheshimu chakula na kukiepusha na viashiria vyote hatari wakati wa kuvisafirisha na kwenye maghala ili kuwaepusha wananchi na athari zinazotokana na chakula kibovu .
Maziwa hayo yenye uzito wa tani 20 yaliingizwa na mfanyabiashara Essak Suleiman wa Darajani tarehe 6  mwezi huu yakiwa yameshaharibika na kuamua kuyazuia yasiingie sokoni.
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa athari zitokanazo na chakula wa ZFDA Asha Suleiman amewashauri wananchi wanapopewa sadaka ya chakula kuwa waangalifu kwani wamegundua baadhi ya wafanyabiashara hutoa sadaka zilizokwisha haribika baada ya kukosa soko.
Aidha amewashauri wananchi wanapokuwa na shaka ya chakula na kuhisi kinadalili ya kuharibika kutoa taarifa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodi ili kwenda kukiangalia na kupata uhakika wake kabala ya kuanza kukitumia.
Wakati huo Mfanyabiashara Essak Suleiman alieingiza maziwa hayo alisema sababu iliyopelekea mzigo huo kuharibika ni upakiaji mbaya uliofanywa na wenye meli, joto kali na kuchelewa kuondoka meli Dubai kuja Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.