Habari za Punde

Wananchi Kisiwani Pemba Wapata Elimu ya Kubaini Changamoto za Elimu Udhalilishaji, Ajira za Watoto na Dawa za Kulevya.

AFISA miradi kutoka shirika la SOS Pemba Ghalib Abdalla Hamad, akizungumza na Wazazi, Walimu wa skuli, mashekhe wa shehia ya Vitongoji Wilaya ya Chake Chake, katika mdahalo wa kubaini changamoto za elimu, udhalilishaji, ajira za watoto na madawa  ya kulevya kwa watoto wa vitongoji, mdahalo huo uliofanyika mjini Chake Chake
MWALIMU wa Skuli ya Msingi Vitongoji Asha Mussa, akitoa changamoto za elimu na mafanikio waliyoyapata, baada ya kikao kilichopita cha walimu, wazazi, mashekhe wa shehia ya Vitongoji na Viongozi wa SOS Pemba, juu ya kujua changamoto za elimu, udhalilishaji, ajira za watoto na madawa ya kulevya kufanyika 
MMOJA ya wananchi wa shehia ya Vitongoji Mariyam Saleh Juma, akichangia katika kikao cha Wazazi, Walimu wa skuli, mashekhe wa shehia ya Vitongoji Wilaya ya Chake Chake, akiwasilisha changamoto za elimu, alizokumbananazo kwa mtoto hadi kuhakikisha amerudi tena skuli

WAZAZI, Walimu wa skuli, mashekhe wa shehia ya Vitongoji Wilaya ya Chake Chake, wakifuatilia kwa makini mdahalo wa kubaini changamoto za elimu, udhalilishaji, ajira za watoto na madawa  ya kulevya kwa watoto wa vitongoji, mdahalo huo uliofanyika mjini Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman- Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.