Habari za Punde

ZIARA YA KITALII MUENDESHA PIKIPIKI KUTOKA NCHI YA OMAN

MUENDESHA Pikipiki kutoka Oman Maher Al Barwany akiingia katika Viwanja vya Wizara Ya Habari Utalii na Mambo ya Kale zilizopo Kikwajuni Mjini Zanzibar kwaajili ya ziara ya kitalii kwa kutumia pikipiki na kufanya mazungumzo na Waziri wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo.
 WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman alipofanya ziara ya kitalii katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
  MSHAURI wa Waziri Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Maalim Abdalla Mwinyi akibadilishana mawazo na Maher Al Barwany  alipofanya ziara ya kitalii katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
  WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman katika ukumbi wa Wizara ya Habari uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar alipofanya ziara ya kitalii Visiwani Zanzibar,  katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
 WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akimvisha Skafu inayotangaza Utalii wa Visiwa Vya Zanzibar Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman katika ukumbi wa Wizara ya Habari uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar alipofanya ziara ya kitalii kushoto ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
 MUENDESHA Pikipiki kutoka Oman Maher Al Barwany akizungumza changamoto na mafanikio katika safari zake alizozifanya kwa kutumia usafiri wa Pikipiki kwa kutalii kulia ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.


WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiendesha Pikipiki linalotumiwa na Maher Al Barwany katika safari zake za kitalii Nchi mbalimbali Duniani (Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.