Habari za Punde

Everton Wawalima ATV Irdning Kwa Mabao 22-0 Mchezo wa Kwanza wa Meneja Marco Silva

Ni mechi ya kwanza ya meneja Marco Silva ambapo goli lilikuwa linafungwa baada ya kila dakika nne huku wachezaji wanne wakifunga kwa njia ya hatitriki.
Wakicheza chini ya Marco Silva kwa mara ya kwanza, Everton hawakuonyesha huruma kwa ATV Irdning waliwanyeshea magoli 22-0
Kevin Mirallas alifunga kwa hatitriki dakika saba za kwanza katika kipindi cha pilii kabla ya kuongeza magoli mawili zaid, washambuliaji Cenk Tosun na Oumar Niasse walifunga mabao manne kila mmoja huki Ademola Lookman alkifunga kwa hatitriki katika kipindi cha kwanza.
Everton walikuwa wamefunga mabao 10-0 wakati wa kipindi cha kwanza lakini wakangeza mengine 12 katika mechi ya kirafiki waliocheza siku chache baada ya wao kutua kwenye kambi ya mazoezi huko Alpine.
Si kwamba Everton walihitaji magoli hayo yote lakini mengine walisaidiwa baada ya ATV Irdning kujifunga ambapo Sebastian Schmidt alijifunga bao la 19 huku la pili lilikuja baada ya Nikola Vlasic kuachwa peke yake golini.
Kikosi cha Silva kinarejea Uingereza kukutana na Bury siku ya Jumatano na kitakumbwa na mtihani mgumu kuliko wa timu ambayo inacheza katika ligi ya tano ya kandanda ya Austria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.