Habari za Punde

Ufaransa Mabingwa wa Kombe la Dunia 2018 Kwa Kufunga Timu Croatia 4-2 Katika Mchezo wa Fainali leo.Modric akosa medali, ajizolea sifa Urusi 2018 Nahodha wa timu ya Croatia iliyofungwa na Ufaransa Modric ni mmoja wa nyota waliong'aa Kombe la Dunia 2018.

Ufaransa mabingwa wa dunia kwa mara yao ya pili tangu 1998. Mnamo 2006 walimaliza nafasi ya pili baada ya kulazwa na Italia. Wamewahi kushika nafasi ya 3 mnamo 1958 na 1986!
Sio leo pekee, Kylian Mbappe amejitambulisha kwenye jukwaa la Urusi kutokana na umahiri wake mechi dhidi ya Argentina kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kasi, chenga za dhihaka na mabao ya maana yaliyoirahisishia Ufaransa kuizima Argentina.Kylian Mbappe ndiye mchezaji wa wa kwanza asiyefikisha miaka 20, tangu shujaa wa Brazil Pele mnamo 1958, kufunga goli katika fainali ya Kombe la Dunia.
Bao alilojifunga huenda limemharibia sifa, lakini alilofunga kuipa Croatia matumaini, limemfanya Mario Mandzukic kumeremeta kwa kuwa mchezaji wa tano kufunga katika fainali ya Kombe la Dunia na Campions league ndani ya msimu mmoja.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.