Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli Awaandalia Dhifa ya Kitaifa Viongozi wa Vyama Vya Siasa Vya Afrika Pamoja na Chama Cha Kikoministi Cha China (CPC) Wanaoshiriki Katika Mkutano wa Viongozi Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Dhifa ya kitaifa aliyowaandalia viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.

Viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC wakiwa katika Dhifa hio ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakiangalia burudani kutoka katika kikundi cha TOT katika Dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Kikundi cha TOT kikitumbuiza katika Dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.