





Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini.
UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro
umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya
abiria ukiwemo kuendesha bila Leseni
,Umri wa kuendesha gari kupitiliza ,
wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.
Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na
yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama Barabarani
,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.
Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na
yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo
Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza
abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .
Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi
wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la
kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva
na wananchi wakipongeza utaratibu huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment