Habari za Punde

Vijana waaswa kuitumia vyema mitandao ya kijamii

Na Takdir Ali,                                 

Vijana nchini wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa mafanikio ili waweze kuibua mambo mazuri yatakayowasaidia katika kuendesha maisha yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwezeshaji Vijana na mabadiliko  (YEC ) Ali Haji Hassan alipokuwa akifunguwa Warsha ya vijana kutoka maeneo mbali mbali ikiwa ni maadhimisho ya kutimia miaka 3 tokea kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo.
Amesema baadhi ya Wananchi watumia vibaya mitandao kwa kufanya mambo maovu kama vile kujiingiza katika vitendo viovu, wizi, kuhamasisha vita,uchochezi na hata wengine kuweka taarifa zao binafsi jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Amefafanua kuwa kitendo cha kutumia vibaya mitandao ya kijamii kinaweza kukuingiza katika matatizo na kupelekea kutokuwa na mustakbali nzuri wa kuendesha maisha yao.
Ameeleza kuwa kuna ongezeko kubwa la Idadi ya Watu hasa Vijana wanaotumia Mitando ya kijamii kama vile Whats app, Tweeter na Facebook, hivyo ni vyema kwa kufanya mambo mazuri kama vile kutangaza biashara na sio kufanya vitendo viovu.
Ameongezea kuwa Tathmini zinaonyesha kuwa mitandao ya kijamii inahamasisha na kushawishi vijana kupiga kura ambapo inasema Idadi ya wapiga kura imeongezeka ukilinganisha na hapo awali kutokana na utumiaji wa mitandao ya kijamii.
"Hebu tuangalie hivi sasa vijana wengi wanapata haki yao ya kikatiba kutokana na ushawishi wa mitando ya kijamii’’,Alisema Mwenyekiti huyo wa YEC.
Aidha amesema Mitando ya kijamii inasaidia katika kutoa fursa za  kupata elimu, habari, mawasiliano, ajira, hivyo ni vyema kwa vijana kuitumia vizur ili iweze kuwapatia manufaa.
Nao washiriki wa warsha hiyo ameipongeza YEC kwa kuandaa Warsha hiyo na kusema itaweza kuwasidia kuepukana na matatizo yanayoweza kusababishw ana matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Akitaja athari kubwa inayoweza kupatikana kutokana na mitandao ya mitandao ya kijamii amesema kuwa ni pamoja na kutumia muda mwingi bila mambo ya msingi, familia kugombana, wizi na utapeli na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
Hata hivyo amewaomba Wanajamii, Viongozi wa vyama vya siasa, Taasisi za Dini na Serikali kushajiisha jamii kuacha kutumia mitandao vibaya.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.