Habari za Punde

WAKILI WA CCM, MBUNGE WAHMIZA VIJANA WA MBEZI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO KWA KUUNDA VIKUNDI NA KUVIRASIMISHA WAKOPESHEKE

Na Bashir Nkoromo
Wakili wa Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwesiga Zaidi na Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha wamewahimiza Vijana kuchangamkia fursa ya mikopo kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuvirasimisha kisheria ili waweze kukopesheka ili kuinua hali zao za kimaisha

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao wamesema, vijana wengi kwa sasa hawakopesheki kwa sababu hawana vikundi na wengi walionavyo havijarasmishwa kiseria hivyo kuwa vigumu kukopesheka na hivyo kubaki wakilalamika tu kwamba serikali ya CCM haiwajali.

Katika semina na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam, Mbunge Msuha ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM , alisema ni lazima vijana kuwa na vipango mizuri ya miradi na kisha kuunda vikundi ili kupata mikopo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo wanayobuni.

"sisi tuliowatangulia tunao uzoefu mkubwa katika masuala ya miradi, ikiwa mnashindwa kubuni wenyewe miradi tufuateni tuwape ushauri nasi tupo tayari wakati wote kwa kuwa maendeleo yenu ndiyo maendeleo ya taifa letu", alisema Msuha katika Semina na Baraza hilo ambalo lilifanyika jana
katika kata hiyo Mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala.

Akihimiza suala hilo katika Baraza hilo na Baraza la Vijana wa CCM tawi la CCM Msumi Centre, Mbezi Mwanasheria huyo wa CCM ambaye pia ni mwanasheria wa Kujitegemea Mwesigwa Zaidi alisema kimsingi CCM haigawi fedha kwa mwananchi yeyote isipokuwa ilichofanya ni kutengeneza fursa ambazo mwananchi yeyote akizitumia vizuri atapata fedha.

"kwa kutambua kuwa ipo haja ya Vijana na Kina mama kusaidiwa katika kuinua vipato vyao imeweka katika katika Katiba yake maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kutenga fedha kutoka katika mapato yake kwa ajili ya kuwakopesha, lakini lazima mjue mikopo hiyo si zawadi, inatolewa kupitia benki na lazima kurejeshwa', alisema Wakili huyo.

Alisema, wakati kinamama wameonekana kunufaika zaidi na fursa hiyo ya mikopo ya serikali ya CCM ambayo kwa sasa inasimamiwa na Rais Dk. John Magufuli, vijana wengi bado hawajanufaika tatizo kubwa likiwa ni kukosa utayari wa kubuni miradi na kuunda vikundi kisha kuvisajili kisheria ili 
wakopesheke.

Wakili Mwesingwa alisema yupo tayari kuwasaidia vijana wa tawi hilo la Msumi Centre katika kusajili vikundi watakavyoanzisha ikiwa ni pamoja na kuwapigia mihuri yake ya uwakili bila malipo.

Mapema katika risala vijana wa Msumi Centre walisema wanao mradi wa kutengeneza chakula cha Kuku wenye gharama ya sh. 444,000 lakini hadi sasa wanazo kibindoni sh. 46,000 tu ambapo katika kujibu risala mwanasheria huyo aliahidi kuwachangia sh. 200,000 ambazo alisema atawapa wiki ijayo.

Wakili huyo pia aliwaasa vijana kuepuka watu wanaotafuta uongozi kwa rushwa badala yake wazingatie maadili ya CCM katika kupata viongozi na pia akahimiza wananchi kusomesha watoto wao ili kuwa chachu iliyo bora zaidi katika kulijenga taifa.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala akizungumza katika Semina na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam, lililofanyika jana katika Kata hiyo. Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Martin Msuha
Katibu wa UVCCM Kata ya Msigani Reihard Chikanda akizungumza wakati wa Semina na Baraza hilo
Katibu wa UVCCM kata ya Msigani Reinhard Chikanda akisoma Risala katika Semina na Baraza hilo
Wajumbe waakiwaa kwenye semina na Baraza hilo
Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (katikati) akisubiri kutoa mada kwenye Semina na Baraza hilo
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mambo kutoka katika makabrasha waliyopewa kwenye Semina na Baraza hilo
Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Martin Msuha akizungumza katika Semina na Baraza hilo.
MSUMI CENTRE⇩
Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (kulia) akipokewa na viongozi wa CCM tawi la Msumi Centre baada ya kuwasili ili kuwa mgeni rasmi katika Baraza kuu ya UVCCM la tawi hilo jana
Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (wapili kushoto) baada ya kuwasili meza kuu katika kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Msumi Centre Omari Mohammed na Wapili kulia ni Mzee wa Baraza la CCM tawi hilo.
Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi akimtuza mtoto Hamisa Mrisho baada ya kufurahishwa na uhodari wa mtoto huyo katika kucheza sarakasi wakati wa Kikao cha baraza hilo.
Kijana wa kikundi cha Vijana wa Msumi Centre akionyesha uhodari wa kuchezea moto
Katibu wa UVCCM tawi la Msumi Centre Justine Najumwe naye akijaribu kuchezea moto
Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Msumi Chetre Omari Mohammed akifungua kikao cha Baraza hilo.
Katibu wa UVCCM tawi la Msumi Justine Najumwe akisoma risala
Katibu wa UVCCM tawi la Msumi Cere Justine Najumwe akimkabidhi risala mgen rasmi Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi
Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi akizungumza wakati wa kikao cha Baraza Kuu la umoja wa Vijana wa CCM tawi la Msumi Centre, Mbezi jijini Dar es Salaam, jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.