Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Wilaya ya Uvinza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua kitalu cha kuzalisha miche ya Michikichi cha Asasi ya Seed Change katika kijiji cha Simbo kwenye jimbo la Kigoma Vijijini Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi  hiyo, Alex Chetkovic
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mazao ya michikichi yaliyokuwa yakikamuliwa  kuwa mafuta ya kula wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma kujionea kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta ya mawese  katika gereza hilko Julai 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojiwa na Ufundi, Profesa Joyce Bdalichako, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni  na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia   wananchi wa kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza alipokuwa safarini  kwenda Uvinza akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma
Wananchi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama kijijini hapa kuwasalimia Julai 29, 2018. Alikuwa njiani kwenda Uvinza kuendelea na ziara ya mkoa wa Kigoma.
(Picha na ofisi ya Waziri MKuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.