Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya Mwenge na Zimamoto Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Zimamoto Imeshinda Bao 2-1.

Beki wa Timu ya Zimamoto kushoto Yussuf Suleiman na Mshambuliaji wa Timu ya Mwenge Yussuf Said wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Zimamoto imeshinda bao 2-1.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu zote zimeonesha mchezo safi na wa kiufundi zaidi kuonesha jinsi wananavyotumia mafunzo ya kocha wao. Timu ya Mwenge imeandika bao lake la kwanza katika dakika ya 34 ya mchezo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Nassor Said. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Timu ya Mwenge ikiwa inaongoza bao 1-0.

Kipindi cha Pili cha mchezo huo Timu ya mwenge itabidi kujilaumu kwa kukosa kutumia nafasi za kuweza kufunga na ili kujiongezea ushindi na mashambulizi yake kutozaa matunda kupitia washambuliaji wao.

Timu ya Zimamoto imeandika bao lake la kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo huo katika dakika ya 50 ya mchezo baada ya mshambuliaji wake kuchezea rafu, adhabu hiyo imeleta matunda kwa timu ya Zimamoto kutoka na shuti kali lililopigwa na mshambuliaji wake Hafadh Bakari. Bao hilo limeubadilisha mchezo huo na kulazimisha Timu ya Zimamoto kuandika bao lake la pili kupitia mshambuliaji wake Hakimu Khamis.
Beki wa Timu ya Zimamoto kushoto Hassan Haji akijaribu kuokoa mpira huku mshambuliaji wa Timu ya Mwenge Nassor Said akijaribu kuchukua mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Zimamoto imeshinda mchezo huo bao 2-1.
Mshambuliaji wa Timu ya Mwenge Seif Pima, akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Zimamoto imeshinda bao 2-1


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.