Habari za Punde

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji.

Na.Mwashungi  Tahir    Maelezo    
MAMLAKA Ya Udhibiti wa Huduma za Maji na 
Nishati ZURA Imeanzisha Baraza la Watumiaji la Zura ili 
kuweza kuwasaidia wananchi  wanaokabiliwa na matatizo ya 
huduma ikiwemo Maji Umeme na Gesi.

Hayo aliyasema huko kwenye Ofisi ya 
Zurailiopo Maisara  mwasilishaji 
MwanasheriaMwandamizi ZURA  Rashid Abdullah 
Fadhil  alipokuwa akiwasilisha madaya Baraza 
laWatumiaji  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi 
wa habari.

Alisema Baraza la Watumiaji la Zura ni Baraza la 
Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa  ambalo  limeanzish
wa chini ya  kifungu Nam 33 cha  sheria ya Mamlaka ya 
Udhibiti wa  Huduma za Maji na Nishati ZURA  Nam 
7.2013. Akielezea lengo la kuanzishwa kwa baraza hilo  ni 
kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Huduma za Maji 
na Nishati  Umeme , Mafuta na Gesi kwa kuwa mtumiaji  anatumia huduma ya maji na 

Nishati mara kwa mara  au ameshawahi kutuma moja ya 
bidhaa zinazodhibitiwa na ZURA.

Aidha alisema kazi za 
BarazalaWatumiaji linatekeleza majukumu yake 
kisheria  kwa kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa 
Hudumazinazidhibitiwa na Zura  kwa kufanya maamuzi , 
kutoa maoni na taarifa   pamoja nakushauriana na Mamlaka , 
pamoja na Wizara husika.

Pia alisema kazi nyengine ya Baraza hilo ni kupokea 
na kusambaza taarifa kuhusu maslahiya watumiaji wa 
Huduma zinazodhibitiwa na Zura  na pia kushauriana na 
wenye viwanda vikubwa , Serikali  na vikundi vya watumiaji 
vya sekta zinazodhibitiwa.

Akifafanua kuhusu njia za kuwasilisha malalamiko 
alisema baada ya kufuata taratibu zote za kuwasilisha 
malalamiko mtumiaji atatakiwa kuwasilisha malamamiko 
moja kwa moja kwenye kitengo cha huduma kwa Wateja  cha 
mtoa Huduma wake.

Vile vile alisema endapo malalamiko 
yake hayatofanyiwa kazi, mlalamikaji anapaswa kuwasilisha 
malalamiko yake ZURA , akipeleka nakala ya barua ya 
malalamiko kwa Baraza la Watumiaji kumuwezesha 
kufuatilia maendeleo ya shauri usika.

Nae Kaimu Mkuu wa Kitengo cha  uhusiano wa Mamlaka 
yaUdhibitiwaHuduma ya Maji na Nishati ZURA  Khuzaimat 
Bakar Kheir aliwatakawananchi  walitumie baraza hilo 
ili kuweza kutatua migogoroyao kwa kupitia mpango maalum .

Pia alisema elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi 
ili waweze kufaidika na baraza hilo ambalo liko kwa ajili 
ya kutatua changamoto za wananchi katika utumiaji wa 
huduma hizo.

Sheria yaZURA kwa kupitia kifungu cha 33 
kkimefafanua uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Watumiaji 
linatakiwa liwe na Wajumbe wasiopungua watano  (5) na 
wasiozidi saba(7) ambao wajumbe hao wanatokana na 
Taasisi zisizo  za Kiserikali ambazo zinatambulika kisheria 
hapaZanzibar ambao watateuliwa na Waziri 
anayeshughulikiaZURA.

Mwisho.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.