Habari za Punde

Kampuni ya Simu za Mkononi Zantel Yatoa Msaada wa Vyakula Kwa Wazee Zanzibar Kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Hajj.

Mmoja wa wazee akipokea msaada wa chakula kutoka kwa mkuu wa Zantel Zanzibar,Mohammed Khamis Mussa (Baucha)
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha)akiongea wakati wa hafla ya kutoa msaada wa chakula kwa wazee.
 Mkurugenzi wa Ustawi wa jamii Zanzibar,Ally Suleiman Abeid, akiongea wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wazee waliohudhuria katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.
Baadhi ya wazee waliopokea msaada katika picha ya pamoja na Mkuu wa Zantel Zanzibar na viongozi wa serikali na Chama Cha Wazee wa Zanzibar.

Na Mwandshi Wetu.
Katika kusheherekea siku kuu ya Eid, kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imetoa msaada wa chakula chenye thamani ya shilingi milioni nane katika kituo cha kutunza wazee cha ‘Amani Sebuleni kwa Wazee’ kilichopo Zanzibar. 

Msaada huo ni mwendelezo wa sera ya kampuni ya Zantel ya kusaidia shughuli za kijamii.

Msaada huo umetolewa katika kipindi hiki cha msimu wa sikuu ya Eid, kinadhihirisha kuwa Zantel inajali makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii inakofanyia biashara zake.

Msaada uliotolewa kwa wazee ni mchele, mafuta ya kupikia,sukari na unga,mbali na msaada huo wafanyakazi wa Zantel walijitoa kusafisha maeneo yanayozunguka kituo hicho cha kutunza wazee.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo.Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) alisema.

“Wakati huu tunaposheherekea sikukuu ya Eid Al Hajj, tunapenda jamii yetu kujisikia kuwa Zantel inawajali watu wote,bila kusahau makundi yenye mahitaji kama wazee, ndio maana tumeamua kutoa msaada wetu katika kituo cha kutunza wazee na kujitoa muda wetu kusafisha maeneo mbalimbali ya kituo hiki”.

Mussa aliongeza kusema kuwa Zantel imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya kusaidia jamii kama vile ya wakulima na wanafunzi lakini katika msimu wa sikukuu hii ya Eid Al Hajj, imetoa msaada kwa wazee ili nao waisherekee kwa furaha.

”Mbali na kutoa msaada wa chakula kwa wazee wa Pemba na Unguja wafanyakazi wameshiriki kufanya usafi maeneo ya kituo cha Sebuleni kuonyesha kuwa wanawajali wazee hao na afya zao kwa kuhakikisha wanaishi katika mazingira safi” alisisitiza.

Msaada huu sio wa kwanza kutolewa na Zantel katika siku za karibuni bali imesaidia makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo Chama Cha Wakulima wa Mazao ya Baharini, Unguja na Pemba, kijulikanacho kama -The Association of Seaweed farmers in Unguja and Pemba, (JUMAMWAZA) ambapo ilitoa msaada wa shilingi milioni 10/- kwa ajili ya kununua pembejeo na vifaa vya kusaidia katika kilimo, msaada huo umenufaisha zaidi ya wakulima 83 wanaoishi katika vijiji vya mwambao wa bahari wanaojihusisha na kilimo hicho.

“Katika kufanikisha sera yetu ya kutumia sehemu ya faida tunayopata kusaidia jamii kwenye maeneo tunayofanyia biashara, katika siku za karibini tumetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Karume pia tumetoa msaada wa Jenereta kwa chuo hicho ili iwasaidie wanafunzi wakati wa mafunzo ya vitendo,” alisema Mussa.

Zantel pia katika siku za karibuni kupitia sera yake ya kusaidia kukabili changamoto za kijamii,ilitoa msaada wa mabati 350 na mifuko 350 ya saruji vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13/- kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyotokea kisiwani Pemba.

Kupitia sera yake ya kusaidia shughuli za kijamii,wafanyakazi wa Zantel hivi karibuni walijitolea muda wao kushiriki kusafisha maeneo ya soko la samaki la Kunduchi jijini Dar es Salaam, ili kuhakikisha mazingira wanayoishi wakati wote yanakuwa safi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.