Habari za Punde

Mafunzo ya Kamati ya Uongozi Makamu,Wenyeviti wa Kamati na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge Yafanyika Afisi za Bunge Zanzibat Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Stephen Kagaigai kulia akitowa maelezo kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano wa Mafunzo ya Kamati ya Uongozi, Makamu, Wenyeviti wa Kamati na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge, kabla ya mkutano huo wakiwa katika chumba cha wageni kulia Naibu Spika  wa Bunge Mhe. Tulia Akson , Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Spika Mstaaf wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa, Spika Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Ameir Pandu Kificho na Mspika Mstaafu wa Tanzina Mhe. Anna Makinda.
Spika Mstaaf wa Tanzania Mhe. Anna Makinda kushoto akizungumza na Waheshimiwa Maspika wakiwa katika chumba cha wageni katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Tunguu Zanzibar, kushoto Spika Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameid Kificho, Spika Mstaaf wa Bunge la Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid. 
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika Mstaaf wa Bunge la Tanzania Mhe. Pius Msekwa alipowasili katika ukumbi wa wageni katika Ofisi za Bunge Tunguu Zanzibar wakihudhuria Mkutano wa Mafunzo ya Kamati za Kudumu za Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akifurahia jambo wakati akisalimiana na Spika Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho. alipowasili katika ukumbi wa wageni katika Afisi za Bunge Tunguu Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.