Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Amtembelea Waziri wa Malisili na Utalii wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Khamis Kigwangala na Msanii wa Mkongwe Mzee Majuto Waliolazwa Hospitali ya Rufaa Muhuimbili Jijini Dar es salaam.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimjulia Hali Waziri wa Malisili na Utalii wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Khamis Kigwangala aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Muhuimbili Jijini Dar es salaam.Dr. Kigwangala amelazwa Hospitali kufuatia kupata ajali akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha akielekea Mkoani Dodoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji  Msanii Mkongwe Nchini Tanzania Mzee Majuto { Maarufu King Majuto} aliyelazwa Wadi wa Sewahaji Hositali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es salaam.Balozi Seif aliwatakia kwa Mwenyezi Mungu Mola wa Viumbe vyote kupona haraka kwa wagonjwa wote wawili ili warejee katika majukumu yao ya kila siku ya kujenga Taifa.
Picha Na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.