Habari za Punde

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar.

Na.Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto Maudline 
Cyrus Castico  amezindua Mabaraza ya Wazee ambapo kwa 
kuanzia Mabaraza hayo yatafanya kazi katika Jimbo la 
Magomeni.

Kuundwa kwa mabaraza hayo kunakusudiwa kuwaweka 
pamoja Wazee hao na kuanzishiwa miradi ya ujasiri amali ya 
kuendeleza maisha yao na kuondokana na umasikini.

Akizindua Mabaraza hayo katika uwanja wa Meya Waziri 
Castico ameitaka Jamii Wazee ipasavyo na kuheshimu 
mawazo yao kwani ndio hazina kubwa kwa Familia na Taifa 
kwa ujumla.

Amefahamisha kuwa Wazee wana haki ya kutoa mawazo yao 
na kusikilizwa kutokana na kujua vitu vingi na uzoefu 
unaotokana na umri mkubwa na utumishi wao.

Waziri Kastiko amesema Wazee hao wametumika muda 
mwingi katika kazi mbalimbali Sekta binafsi na Serikali 
ikiwemo Uhasibu na Nyanja mbalimbali za ulinzi hivyo 
mawazo yao ni muhimu.

Aliongeza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza 
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amewapa kipaumbele 
katika Serikali yake na huwapa pencheni ya kila mwezi ili 
kujikimu mahitaji yao bila ubaguzi.

Amesisitiza kuwa Wizara yake iko makini katika kuhakikisha 
wazee wote wanakuwa na mazingira mazuri ya kuwapatiwa 
mambo muhimu yanayohitajika ikiwemo matunzo ya 
uhakika na malezi bora.

“Wizara yangu iko mstari wa mbele kwa kuwalinda wazee 
kwani wao ndio wenye fikira na busara katika kupanga 
mambo ya maendeleo yao” .Alisema Waziri huyo.

Hata hivyo aliwasihi wazee hao kuzidisha mashirikiano na 
kusaidia kuweka mikakati ya kupambana na vitendo vya 
udhalilishaji ambavyo vimekithiri katika jamii.

Sambamba na hayo viongozi wa jimbo hilo akiwemo mbunge 
Jamal Kassim Ali na Mwakilishi Rashid Makame Shamsi 
wameahidi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wazee hao na 
kuwapatia huduma za afya.

Viongozi hao pia wameahidi kuwa karibu nao na kupokea 
fikra na busara zao kwa kwa faida yao na Jimbo kwa ujumla.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.