Habari za Punde

Yaliyojiri Leo Agosti 6, 2018 Mkutano Wa Rais Dk Shein Na Waandishi Wa Habari Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Abeid Amani Karume

YALIYOJIRI LEO AGOSTI  6, 2018  MKUTANO WA RAIS DK SHEIN NA WAANDISHI WA HABARI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME

RAIS MHE DK SHEIN
#  Ziara yangu ya Indonesia  ilijielekeza katika sekta zifuatazo, Kilimo, Biashara na Kilimo, Uwekezaji, Ushirikiano baina ya Nchi mbili hizi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

#  Sekta ya Kilimo tulizungumzia suala zima la maendeleo ya kilimo cha Minazi, kilimo cha Mwani na kuusarifu mwani na kuangalia kilimo cha Mpunga.

#  Utalii tulizungumza juu ya utalii wenyewe na mwelekeo wake, elimu kuhusu Utalii na Kampuni inayowekeza kuhusu utalii. Tulizungumza na kupata uzoefu wao.

# tulitembelea Viwanda vya samaki tukapata uzoefu wao na kupata mwelekeo mzuri wa kazi zao.

#  Tulizungum,za pia na Wafanya biashara wa Indonesia na kuwahamasisha kuja kuwekeza Zanzibar.

# Tulizungumza pia Kampuni ya Gesi nao wanahamu ya kuja kuwekeza Zanzibar katika Suala la  kutafuta na kuchimba Gesi.

# Tulitembelea na kuona namna Mwani unavyosarifiwa na kuleta faida kwa Wakulima.

#  Katika wiki mbili zinazokuja Wawekezaji katika kilimo cha Mwani watakuja na kufanya mazungumzo na ikibidi watusaidie kuweka hata kiwanda kidogo cha Kusarifu mwani ili kuleta tija kwa Wananchi.

# Wameahidi kutusaidia sana katika uwekezaji, Mafunzo ya watendaji wetu na kuongeza Idadi ya WAtalii watakokuja kuitembelea Zanzibar.

# Tulikubaliana namna ya kushirikiana na kupeana uzoefu baina ya Chuo chao cha Utalii na Chuo kikuu  chetu cha SUZA.

# Tumekubaliana pia kupeleka Madaktari wetu katika Kituo kikuu kinachotumika kutibu maradhi ya Moyo ambapo tumekubaliana kupeleka Madaktari wetu huko wakapate uzoefu na wakwao pia waje kwetu kutufundisha.

# Siku za karibuni Ujumbe kutoka Indonesia utakuja hapa Zanzibar na kuja kufanya mazungumzo kupitia Bank yao ya Exim 

# Kiujumla Watu wa Indonesia wakiwemo Viongozi na Wawekezaji wamefurahishwa na Zanzibar na wako tayari kuja Zanzibar hivyo ni jukumu letu kuwaalika ili kuleta mafanikio tunayotarajia.

#  Watendaji wakuu niliofuatana nao nao pia watapata nafasi ya kuzungumza kwa undani kile ambacho tulikiona na kujifunza.

# Watu wako tayari kuisaidia Zanzibar hivyo ni vyema nasi kuweka mazingira mazuri ya kusaidiwa.

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR
AGOSTI 6, 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.