RAYA HAMAD (ORKSUUUB)
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria
utumishi wa umma na Utawala Bora Mh Haroun Ali Suleiman amezitaka taasisi za
kisheria zilizomo ndani ya Ofisi hio wakiwemo majaji , mahakimu na wanasheria
kufanya kazi kwa mashirikiano ili jamii iweze kuelewa na kufahamu masuala ya
sheria na kuwaepushia usumbufu wananchi .
Haroun amesema matatizo mengi ya
kisheria yanaweza kupunguwa kwa
kufanyiwa kazi iwapo watendaji watakuwa na utaratibu wa kuwafuata wanajamii
waliko kwa kuwapa elimu ikiwa ni pamoja na kutumia vyombo vya habari mbali
mbali .
Aidha amewasiitiza viongozi wa Tume ya
Kurekekebisha sheria na Tume ya Utumishi
wa Mahakama kulipa kipaubele suala la elimu kwa kusomesha watendaji wake pia
kuendeleza uhusiano mwema wa kimataifa na nchi nyengine kwa lengo la kujenga
uelewa zaidi na ushirikiano mwema kwa mataifa ya nje.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha
sheria Jaji Mshibe Ali Bakari ameitaka jamii kufatilia kwa karibu masuala ya sheria
ili kuepusha migongano isiyo ya lazima “hivi
sasa tumeanza kuwafikia wanajamii waliko awali wananchi walikuwa na khofu ya
kutoa maoni yao kuhusiana na sheria hii ilitokana na uwelewa mdogo waliokuwa
nao ”alisisitiza Jaji Mshibe.
Akiwasilisha taarifa ya Tume hio Kaimu
katibu ndugu Ali Juma Ali amesema kuwa Tume inawajibu wa kupendekeza mabadiliko
ya sheria kwa mujibu wa mazingira ya Zanzibar ,kuhakikisha kuwa sheria zinatoa
haki na usawa ,kutoa elimu kwa wananchi ili wapate uwelewa wa sheria zao ,kutafsiri
sheria ili zifahamike kwa wanajamii, kushauri njia mpya za utekelezaji wa
sheria, kuziweka pamoja sheria za Zanzibar, kuimarisha mashirikiano na
taasisiza kimataifa zenye majukumu sawa na Tume
pia kuchapisha makala ya sheria za kimataifa ndani ya Zanzibar , ikiwa
makala hayo yanakwenda sambamba na maadili ya mzanzibari.
Wakati huo huo Waziri Haroun ameitaka Tume ya Utumishi Serikalini kuhakikisha inawahakiki
waajiriwa kabla kuwaajiri jambo ambalo inatengeneza nidhamu ya kazi uwajibikaji na maadili ili kuwapata watumishi wenye nia na moyo wa
kizalendo kwa maslahi ya nchi
Haroun amesema Tume ndio inayojenga nidhamu
na maadili Serikalini hivyo itakapochaguwa wajiiri wasio na uwezo na maadili ya
kazi itakuwa imekiuka misingi na
taratibu za uajiri “inasikitisha kuona kuwa wafanyakazi wanafukuzwa kila mwaka
kwa utovu wa nidhamu,kukosa uzalendo na sifa za kiutendaji .
Amewaasa wajumbe hao kutojihusisha na
masuala ya kupokea rushwa au kushutumiwa kwa kukiuka taratibu za kiuajiri kwa
waombaji ambao hawatakuwa na sifa na
badala yake wakaingizwa kazini kwa upendeleo au rushwa hilo halitavumilika .
Nae Mwenyekiti wa Tume hio Kombo Hassan Juma ameomba kupatikana kwa ofisi ya
kufanyia kazi badala ya kutumia jengo waliopo hivi sasa la People Palace
ambalo mazingira yake hayako vizuri kiutendaji
pia kulipa umuhimu wa historia ya kipekee
iliyopo katika Ofisi hizo ambazo hivi karibuni jengo hilo litafanyiwa
marekebisho.
Katika risala iliyosomwa na Katibu wa Tume
hio ndugu Mohammed Khamis amesema kuwa Tume
inamamlaka ya kuajiri watumishi wapya , kuthibitisha kazini watumishi ,
kuidhinisha nyongeza za muda wa utumishi , ajiira za mikataba , kupandisha
daraja , kuidhinisha kustaafu kazi kwa watumishi waliofika umri wa kustaafu
kazi kwa watumishi waliofikia umri wa kustaafu kazi kwa lazima , kustaafu kwa
maradhi na kustaafu kwa hiari, kubadilisha kada na kuacha kazi.
Aidha Tume ina wajibu wa kusimamia haki na
nidhamu za watumishi walio chini ya usimamizi wa tume ikiwa ni pamoja na
kuidhinisha kufukuzwa kazi watumishi waliokwenda kinyume na sheria, kanuni na
taratibu za utumishi , kupokea
kusikiliza na kuyatolea maamuzi sahihi malalamiko na rufaa zote
zinazowasilishwa baada ya kuzingatiwa taratibu zote kwa mujibu wa sheria na kanuni .
Akielezea mafanikio ya Tume hio Bw Mohammed
amesema katika mwaka 2017/ 2018 Tume
imeajiri vijana 2968 kwa Unguja na Pemba kati yao 2023 walikuwa ni wanawake sawa
na asilimia 68.2 na wanaume 945 sawa na asilimia 31.8 ambapo kwa kipindi cha
mwaka wa fedha 2017/2018 Tume ilipokea
jumla ya maombi ya kazi 29774 ambapo pia Tume imeidhinisha kufukuzwa kwa kazi
watumishi 129 kutokana na makosa mbali mbali ya utovu wanidhamu hasa utoro
kazini
Nae
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi wa umma na Utawala Bora Nd
Yakout Hassan Yakout amesema lengo la ziara hio ni kuangalia mazingira ya kazi
na fursa za watendaji , changamoto na mafanikio
Wafanyakazi wa Tume hio wameahidi kuendelea
kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na mazingira magumu waliyonayo
Mhe Haroun ameizindua Tume ya Utumishi
Serikalini ambapo imeanzishwa kwa mujibu
wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 117 toleo la mwaka 2016 sambamba
na kifungu 33cha sheria ya sheria Utumishi wa Umma No. 2 ya mwaka 2011 .
No comments:
Post a Comment