Habari za Punde

Nafasi za kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR


Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kama ifuatavyo:-

1.Mhandisi Ujenzi (Civil Engineers) Daraja la II “Nafasi 3” – Unguja 
“Nafasi 2 Pemba”

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Muhandisi Ujenzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Msanifu Majengo (Architect Building) Daraja la II “Nafasi 2” -Unguja na “Nafasi 2” - Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Msanifu Majengo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Mthamini Majengo (Qualtity Surveyor) Daraja la II “Nafasi 1” – Unguja na “Nafasi 1” - Pemba

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mthamini Majengo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4.Mhandisi Umeme (Electrical Engineer) Daraja la II “Nafasi 1” – Unguja 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhandisi Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

5.Mhandisi Computer (Computer Engineer) Daraja la II “Nafasi 1” - Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani Mhandisi Computer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

6.Mhandisi Mashine (Mechanical Engineer) Daraja la II “Nafasi 1” – Unguja 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
.Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani Mhandisi Mashine kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

7.Fundi Sanifu Ujenzi (Civil Engineer)) Daraja la II “Nafasi 2” – Unguja “Nafasi 2 Pemba”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Fundi Sanifu Ujenzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-


KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 13 Septemba, 2018 wakati wa saa za kazi.

•Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti WWW.LPS.GO.TZ

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.