Habari za Punde

Serikali ya Oman Yakabidhi Mashine za Kisasa za Kuhifadhia Nyaraka na Kumbukumbu Kwa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar.

Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilimani Zanzibar. 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akionesha hati za makabidhiano ya Mitambo ya kutunzia Nyaraka na Mwenyekiti wa Mamlaka yay a Uhifadhi Nyaraka na Makumbusho wa Serikali ya Oman, Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyan kulia, wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano iliofanyika katika Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilimani Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akitowa shukrani baada ya kukabidhiwa Mashine za Kisasa za kuhifadhia Nyaraka na Mwenyekiti wa Mamlaka yay a Uhifadhi Nyaraka na Makumbusho wa Serikali ya Oman, Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyan, baada ya hafla ya makabidhiano yaliofanyika katika Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kushoto Balozi Mdogo wa Oman anayafania kazi zake Zanzibar.
Mwenyekiti wa Mamlaka yay a Uhifadhi Nyaraka na Makumbusho wa Serikali ya Oman, Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyan, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya Mashine za kuhifadhi Nyaraka, katika ukumbi wa ofisi hizo kilimani Zanzibar.
Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia kazi zake Zanzibar akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidho vifaa hivyo kwa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar katika majengo ya taasisi hiyo kilimani Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na kutowa shukrani kwa Serikali ya Oman kwa msada wao huo wa mashine za kuhifadhia Nyaraka na Kumbukumbu, Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo Kilimani Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar na Waziri wake Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.  
Mtaalamu wa kuhifadhi Nyaraka wa kutoka Mamlaka ya Uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa Oman Mohammed Al Sulaim, akitowa maelezo jinsi ya kuhifadhi Nyaraka kupita mitambo hiyo wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilmani Zanzibar.
MWENYEKITI wa Mamlaka ya Uhifadhi Nyaraka na Makubusho wa Serikali ya Oman Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyan, akitowa maelezo ya Mitambo ya kuhifadhia Nyaraka, kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilimani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.