Habari za Punde

Tamasha la Bonaza la Kombe la Ujamaa Sports Club Zanzibar Kati ya Taifa ya Jangombe na Gulioni City Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe Imeshinda Mchezo Huo Kwa Bao 3-0.

Mshambuliaji wa Timu ya Gulioni City Shaban Mohammed akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakati wa Mchezo wao wa Kuwania Kombe la Ujamaa Sports Club kuadhimisha Miaka 61 Tangu kuazishwa kwa Timu hiyo mchezo uliofanyika  Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda kwa bao 3-0.

Timu ya Taifa ya Jangombe imesonga mbele baada ya kuotoa Timu ya Gulioni City katika kundi B la muchuano hiyo kuwania Kombe la Ujamaa Bonaza kuadhimisha Miaka 61, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 

Timu ya Taifa ya Jangombe imeonesha mchezo wa kiwango cha juu  na kumiliki idara zote uwanja katika dakika tisini za mchezo huo na kuweza kuongoza bao lake la kwanza katika dakika ya tatu ya mchezo huo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Mohammed Omar baada ya kuwapita mabeki wa Gulioni City na kuipatia timu yake bao hilo.

Mshambuliaji Mohammed Omar ameonesha mchezo safi na kuwa tishio kwa timu ya Gulioni City kwa kuwapita mara kwa mara ngome hiyo, katika dakika ya 12 ya mchezo huo mshambuliaji wake Said Mussa ameipatia Taifa ya Jangombe bao la Pili na baada ya dakika kumi za mchezo huo Said Mussa ameweza kuipata Timu yake ya Taifa ya Jangombe bao la tatu na kufunga karamu ya mabao katika mchezo huo.

Muchuano hiyo itaendeleo leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuzikutanisha Timu za Malindi na Mchangani AFC, katika majira ya jioni saa 10:00. 
Mshambuliaji wa Timu ya Gulioni City akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakati wa mchezo wa Tamasha la Bonaza la Kombe la Ujamaa Sports Club mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda mchezo huo bao 3-0.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe na Gulioni City wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Ujamaa Sports Club uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda mchezo huo bao 3-0. 
Viongozi wa benchi la ufundi la Timu ya Gulioni City wakiwa na majonzi wakati timu yao ikiwa tayari imeshapata kipigo na kuyaaga mashindano ya Kombe la Ujamaa Sports Club kuadhimisha miaka 61 ya Timu hiyo Tangu kuazishwa kwake mwaka 1957 Zanzibar.
Muamuzi wa mchezo huo akimuagalia mchezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe baada ya kuchezewa faulu na mchezaji wa Timu ya Gulioni City.
Wachezaji wa Timu ya Gulioni na Taifa ya Jangombe wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Ujamaa Sports Club mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe akiwapita mabeki wa Timu ya Gulioni City wakati wa mchezo wao wa Kombe la Bonaza la Ujamaa Sports Club mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0. 
Wachezaji wa Timu ya Gulioni City wakitafakari baada ya kumalizika kipindi cha kwanza cha mchezo huo tayari wakiwa nyuma kwa mabao 3-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Jangombe mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuwania Kombe la Bonaza la Ujamaa Sports Club Zanzibar kutimia miaka 61 ya Timu hiyo.kongwe Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.